Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi (SACP) Janaeth Magomi akiwapongeza wananchi kwa kutoa Nyumba ili itumike kwa matumizi ya awali kama Kituo kidogo cha Polisi cha Kata ya Mhongolo Wilayani Kahama Mkoa wa Shinyanga.
Na Mwandishi wetu Malunde 1 Blog.
Katika kukabiliana na vitendo vya kihalifu wananchi wa Kata ya Mhongolo Wilayani Kahama Mkoa wa Shinyanga wameamua kutoa nyumba ili itumike kwa matumizi ya awali kama Kituo kidogo cha Polisi wakati wakiendelea na jitihada za kutafuta eneo kwa ajili ya ujenzi wa Kituo cha Polisi jambo litakalo saidia kupunguza Vitendo vya Uhalifu na adha ya kutafuta huduma hiyo umbali mrefu.
Wananchi hao wamesema hayo leo Desemba 18, 2024 wakati wa uzinduzi wa kituo hicho ambapo wameeleza lengo la kufanya hivyo nikutokana na Kata hiyo kutokuwa na kituo cha Polisi sambamba na kutokuwa na usalama katika maeneo yao kutokana na mwingiliano wa watu kutoka maeneo mbalimbali waliofika kwa ajili ya shughuli za kiuchumi.
Akizungumza wakati akizindua kituo hicho Kamanda wa Polisi Mkoa wa Shinyanga Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi (SACP) Janaeth Magomi amewashukuru wananchi hao wakiongozwa na wafanyabiashara, wadau na vikundi vya Ulinzi shirikishi kuwezesha kupatikana kwa kituo hicho ambacho kitaongeza ufanisi wa kazi wa Jeshi la Polisi katika kuwahudumia wananchi.
Kwa upande wake Afisa Mtendaji wa Mtaa wa Mhongolo Rita Modest amewataka wananchi wa Kata hiyo kutumia kituo hicho kuripoti matukio ya kihalifu ili Mkoa huo uendele kubaki salama.
Tazama picha hapa chini👇
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Shinyanga Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi (SACP) Janeth Magomi akiwapongeza na kuwawashukuru wakazi wa mtaa wa Mhongolo kwa kutoa nyumba ili itumike kama kituo cha polisi.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Shinyanga Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi (SACP) Janeth Magomi akiwapongeza na kuwawashukuru wakazi wa mtaa wa Mhongolo kwa kutoa nyumba ili itumike kama kituo cha polisi.
Social Plugin