Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

RUN FOR BINTI MARATHON YABORESHA MAZINGIRA YA SHULE NA JAMII YA MTWARA


Mbio za hisani za “Run for Binti Marathon” ambazo hufanyika mwanzoni mwa mwaka zenye lengo la kuboresha Mazingira ya Elimu na afya kwa wanafunzi wanaosoma katika maeneo yaliyopo pembezoni mwa nchi zimefanikiwa kuboresha mazingira ya shule ya Sekondari Mnyawi iliyopo, Mtwara, kwa kujenga vyoo vya kisasa vyenye matundu 12 kwa matumizi ya wavulana na wasichana.

Aidha, mabinti wa shule hiyo wamepokea taulo za kike zinazoweza kutumika tena (reusable pads) zipatazo kwa wanafunzi wa kike zaidi ya 200 hatua inayolenga kuimarisha afya na usafi wa wanafunzi wa kike.

Mbio hizi pia zilihusisha utoaji wa elimu muhimu kwa wanafunzi na jamii ya Mtwara kupitia wadau mbalimbali wakiwemo Stanbic Bank Tanzania, Marie Stopes Tanzania, na Girl Guide Tanzania ambapo jamii na wanafunzi wamepewa elimu juu ya maswala ya Ukatili wa kijinsia, elimu ya fedha , hedhi salama na afya ya uzazi , utunzaji wa mazingira ikiwemo kupata miti pamoja na mafunzo kuhusu nishati safi. 

Mbio za Run for Binti zinaratimiwa na Smile for Community kwa kushirikiana na LSF kila mwaka kwa miaka mitatu sasa.

Akiongea kuhusu mchango huo kwa jamii kupitioa mbio za Run for Binti , Mkurugenzi mkuu wa Runf for Binti Bi Flora Njelekela amesema msimu wa pili na watatu wambio hizi umekuwa ukifikia jamii ya mkoa wa Mtwara Mbio za Mwaka jana ziliwafikia shule ya sekondari Nanyamba na kwa mwaka huu shule hii ya sekondari ya Mnyawi ambapo tutakabidhi choo chenye matundu 12 kwa watoto wakike na wakiume, kupanda miti pamoja na taulo za kike. Mchango huu umeboresha mazingira na utoaji elimu, afya bora kwa ujumla. Napenda kuwashukuru wadau wote waliotuunga mkono katika mbio za mwaka huu 2024.

Mgeni rasmi mkuu wa Mkoa wa Wilaya ya Mtwara, Abdallah Mwaipaya, aliwashukuru wadau kwa kufanikisha miradi hiyo nakupongeza juhudi zinazofanya na wadau katika kutatua changamoto za jamii ikiwemo wakazi wa mkoa wa Mtwara.

"Nawashukuru sana wadau kwa kuchagua Mtwara kama sehemu ya kutekeleza miradi hii muhimu. Maboresho haya yatanufaisha wanafunzi na jamii nzima ya Mtwara. Tunawakaribisha kuendelea kuwekeza katika miradi mingine ya maendeleo. Nitumie fuslsa hii kuwahasa jamii kutumia fulsa hii vizuri na mafunzo mliyoyapata yakapunguze changamoto zilipo ikiwemo matatizo ya ndoa na kuwalinda wanawake na kuwashirikisha katika shughli za kiuchumi na maamuzi. Aidha nitoe rahi kwa shule kutunza na kukuza miti tuliyoipanda leo na kutunza miundo mbinu tunayokabithi leo.

Kwa upande wake mwakilishi wa LSF Bi Jane Matinde amewashukuru wadua wote waliounga mkono mbio hii kwa mwaka huu iliyowezesha kutoa mchango huu mkubwa kwa wakazi wa mnyawi na Mtwara kwa ujumla na kutangaza maandalizi ya Mbio Za Run for Binti 2025 yameanza Rasmi na mbio hizi zinagembea kukimbia wiki ya hedhi salama.

Aidha Bi Doreen Dominic Mkuu wa kitengo cha Biasha Stanbic Bank na wadhamini wa kuu wa mbio za run for binti amesema "Kama Stanbic Bank, tunaamini katika kurudisha kwa jamii. Uwekezaji wetu katika maswala ya kifedha, mazingira , elimu na afya ya watoto wa kike ni sehemu ya juhudi za kusaidia kukuza kizazi kijacho chenye maarifa na afya bora lakini pia jamii yenye maisha bora bila kumwacha mtoto wa kiume nyuma na ndo maana mchango wetu unawalenga makundi yote hasa yaliyo pembezoni.

Mbio za Run for Binit Mwaka 2024 zimedhaminiwa na wadau mbalimbali ikiwemo Stanbic Bank, Songas, East Africa Law Society, Azam Media, Girl Guide Tanzania, Maria stopes, NMB bank,Kilimanjaro water, SGA security, Mlimani City, Tronix generator , SGA Security, Msichana initiatives, Sxulit Army na zaidi washiriki 800 walishiriki na kuchangia mbio hizi

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com