Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

RUTAINIRWA KUANZA KUTOA DARASA LA MATUMIZI YA VYOO VILIVYOUNGANISHWA MFUMO WA MAJI TAKA


Na Dotto Kwilasa, DODOMA

Mwenyekiti wa Serikali ya mtaa wa Nyerere kata ya Kilimani Jijini Dodoma Lussy Rutainirwa anatarajia kuanza ziara ya kikazi na wajumbe wake kupita nyumba kwa nyumba kwa lengo la kutoa elimu ya kuondokana na chemba za vyoo ambazo bado hazijaunganishwa katika mfumo wa maji taka kutoka mamlaka ya maji safi na usafi wa mazingira (DUWASA)

Kauli hiyo ya mwenyekiti wa mtaa wa Nyerere Lussy Rutainirwa ameitoa wakati akiongea na kituo hichi juu ya kuwepo kwa chemba nyingi ambazo hazijaunganishwa katika mfumo wa maji taka na mamlaka ya maji safi na usafi wa mazingira DUWASA.

"Katika mtaa wangu wa Nyerere bado kaya nyingi zinatumia mfumo wa kizamami wa kuchimba na kujenga chemba za kuhifadhia maji taka jambo hili limekwisha kupitwa na wakati"amesema mwenyekiti Rutainirwa

Aidha mwenyekiti huyo amesema katika kipindi hichi cha mvua za masika chemba nyingi huwa zinajaa na kufurika hivyo huatarisha maisha ya wananchi wangu hasa watoto wanapokuwa wakicheza husababisha magonjwa ya kuhara kama vile kipindupindu.

Rutainirwa amesema katika ahadi zake wakati akiwaomba ridhaa wana mtaa wa Nyerere alisema swala lake la kwanza alipo ingia madarakani ni kuanza na hili swala la chemba kuhakikisha wanatoa elimu kwa wakazi wote wa mtaa wa Nyerere ili kuweza kuwasaidia kuwaunganishia chemba zao katika mfumo wa maji taka unaotekelezwa na Duwasa kuhakikisha mfumo huo unapeleka maji taka moja kwa moja kwenye bwawa la swasawa jijini Dodoma.

Nilikutana na wajumbe wangu na kushauriana nao ili kwa pamoja tuanze ziara ya nyumba kwa nyumba kwa lengo moja tu kwanza la kutoa elimu umuhimu wa kujiunga kwenye mifumo huo wa maji taka na kuondokana na chemba katika nyumba zao kwakuwa hata chemba zikijaa wanatumia garama kubwa kunyonya kuliko wakijiunga watatumia garama ndogo.

Aidha mwenyekiti Rutainirwa amesema wakisha maliza kutoa elimu hiyo sasa watakwenda Duwasa kwaajili ya utekelezaji kwakuwa watakuwa na idadi kamili ya kaya ngapi zinajiunga katika mfumo huo.




Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com