Katika kipindi cha miaka mitatu ya uongozi wa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan, serikali yake imetoa kiasi cha shilingi trilioni 2.53 kwa ajili ya uboreshaji wa miundombinu ya barabara vijijini.
Kwa mujibu wa muhtasari wa mafanikio ya miaka mitatu ya Serikali ya Awamu ya Sita inayoongozwa na Rais Samia tangu aingie madarakani uliotolewa na Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), Wakala ya Barabara Vijijini (TARURA) imefanikiwa kujenga barabara za lami za urefu wa kilomita 819.22.
Ujenzi huo umeongeza mtandao wa barabara za kutoka Kilometa 2,404.90 hadi kilometa 3,224.12.
Aidha ujenzi wa barabara za changarawe ni Kilometa 11,924.36 na kuongezeka kwa Mtandao wa barabara za changarawe kutoka Kilometa 29,183.17 hadi kilometa 41,107.52
Ujenzi wa Madaraja ambayo yamekamilika, wakala imejenga madaraja makubwa sita (6) ambayo ni ya Berega (140m) -(Kilosa,) Msadya (60m) -(Mpimbwe DC), Mwasanga (40m)- (Mbeya) ya mejengwa na yanatumika.
Aidha ujenzi wa madaraja ya Kiwila-(40m)-Ileje, Mkomanzi-Korogwe (60m) na Kalambo (80m)-(Kalambo), unaendelea kukamilishwa.
Pia kumekuwa na jitihada za kutekeleza ujenzi wa barabara na madaraja kwa kutumia malighafi za ujenzi zinazopatikana katika maeneo ya kazi zinapotekelezwa.
Ujenzi wa barabara kwa kutumia mawe - Mpaka sasa jumla ya kilometa 23.18 za Barabara ya Mawe zimejengwa kwa gharama ya Tshs bilioni 8.1 ambapo ni sawa na Tshs. bilioni 12.8 kama ingetumika lami nyepesi (double surface dressing) na Tshs. bilioni 33.6 kama ingetumika lami ya zege (Asphat Concrete)
Ujenzi wa madaraja kwa kutumia mawe ni mojawapo ya kipaumbele cha TARURA ikiwa ni pamoja na kutumia malighafi zinazopatikana maeneo ya kazi ili kupata ufanisi wa gharama za ujenzi.
Hadi Mwezi Februari, 2024 TARURA imejenga madaraja 226 ya mawe yenye thamani ya Shilingi bilioni 12.52 ambapo gharama imepungua kwa zaidi ya asilimia 50.
Social Plugin