Agizo hilo limetolewa Jijini Dodoma Disemba 19,2024 na Naibu Katibu Mkuu, Wizara ya Fedha, Jenifa Omolo, kwa niaba ya Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Dkt. Natu Elmaamry Mwamba, wakati akifungua kikao cha kuimarisha ushirikiano kati Serikali ya Mapinduzi Zanzibar na Tanzania Bara kuhusu masuala ya Ubia Kati ya Sekta ya Umma na Sekta Binafsi-PPP.
Amesema utekelezaji wa miradi kupitia PPP ni sehemu ya kujenga uchumi imara na ni suala linalotekelezwa na nchi nyingi duniani.
Kwa upande wake Naibu Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais, Kazi, Uchumi na Uwekezaji, Zanzibar, Rashid Ali Salim, amewaagiza wataalam hao kuyafanyia kazi yote waliyokubaliana hususani suala la kuwa na mkakati wa pamoja wa kuuza fursa na kuibua miradi ya pamoja ya PPP ili kuimarisha sekta ya PPP nchini.
Kaimu Kamishna wa Kitengo cha Ubia Kati ya Sekta ya Umma na Sekta Binafsi-PPP, Wizara ya Fedha, Bashiru Taratibu, amesema wamejadili kuhusu miradi ya pamoja ambayo Sekta Binafsi inaweza kutekeleza kama mradi wa Daraja la Dar es Salaam hadi Zanzibar, lakini kila sehemu wana Sheria yao ya PPP, kwa hiyo wanatafuta namna bora ya kutekeleza suala hilo iwapo mwekezaji atajitokeza.
Kwa upande wake, Mkurugenzi Mtendaji wa Kituo cha Ubia Kati ya Sekta ya Umma na Sekta Binafsi-PPPC, David Kafulila, amesema wamejadiliana mambo mbalimbali ya kurahisisha suala la ubia nchini ili kuipunguzia mzigo Serikali wa kugharamia miradi ya maendeleo ambayo inaweza kugharamiwa kupitia PPP.
Tanzania kwa sasa inafanya vizuri katika eneo la PPP ambapo kwa Tanzania Bara kuna takribani miradi 74 ambayo ipo katika hatua za mwisho kuanza kutekelezwa na Zanzibar kuna zaidi ya miradi 13.
Social Plugin