******
Serikali ya Tanzania imesema imeweka mikakati ya kina kwa ajili ya kujenga uwezo wa mfumo wa afya, ikiwa ni pamoja na kuidhinisha ushirikiano kati ya sekta ya umma na binafsi.
Alisema Mradi huo wa IMECT wenye thamani ya TZS
Bilioni 1.8 ni mfano bora wa mafanikio ya ushirikiano, ukileta pamoja Serikali
ya Tanzania, washirika wa kimataifa, na jamii za ndani katika jitihada za
kuimarisha huduma za matibabu ya dharura kote nchini.
Natumia fursa hii kuishukuru Serikali ya Poland
kupitia Kituo cha Msaada wa Kimataifa cha Poland (PCPM) na Huduma za Afya Aga
Khan Tanzania (AKHST) kwa hatua kubwa waliyopiga ya kutambua hitaji na kutoa
ufadhili wa kiasi cha dola za Marekani 760,000, sawa na shilingi za Kitanzania
bilioni 1.8, kwa lengo la kuboresha huduma za dharura nchini katika kipindi cha
miaka miwili na nusu iliyopita.”
Pia alipongeza huduma za Afya za Aga Khan Tanzania kwakuwa ni mfano wa kuigwa katika ushirikiano wa sekta ya Umma na Binafsi kwa juhudi zake za kusaidia juhudi za serikali katika kuimarisha mifumo ya afya.
Kwa upande wake Waziri wa mambo ya nje wa Jamhuri ya
Poland Jakub Wisniewski alisema wanafuraha kushirikiana na serikali ya Tanzania
kupitia Taasisi ya Huduma za afya ili kuimarisha huduma hizo za dharura
Naye Mratibu wa Huduma za Dharura na Utunzaji Muhimu kutoka Wizara ya Afya, Dkt. Erasto Sylvanus, aliishukuru timu za usimamizi wa vituo vyote vilivyoshirikiana kwa uongozi na msaada wao wakati wa utekelezaji wa mradi.
"Naipongeza Serikali ya Tanzania, kupitia Mheshimiwa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan, kwa kuunga mkono ushirikiano wa sekta nyingi kati ya umma na binafsi ili kushughulikia mahitaji ya jamii na mifumo ya afya."
Dkt. Hussein K. Manji, Mratibu wa Mradi, Taasisi ya Huduma za Afya ya Aga Khan Tanzania alisema: "Fani ya Magonjwa za Dharura ni taaluma maalum yenyewe, na haitoshi tu kujua la kufanya, bali pia kuwa na rasilimali na uwezo wa kutumia ujuzi huo kwa vitendo ni muhimu. Tunapojenga uwezo na kuimarisha miundombinu, tunalenga kupunguza rufaa,kupunguza vifo, na kuwapa wananchi wetu walioko katika hali mbaya nafasi bora zaidi ya kupona."
——MWISHO—-
Social Plugin