Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

TANESCO SHINYANGA YAZINDUA BONANZA LA PEPMIS 2024

Na Mwandishi wetu - Malunde 1 blog

Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) Mkoa wa Shinyanga limezindua rasmi bonanza la matumizi ya Mfumo wa Utendaji na Ufuatiliaji wa Majukumu ya Watumishi wa Umma (PEPMIS) kwa watumishi wake.

Bonanza hilo limefanyika leo, Desemba 14, 2024, katika uwanja wa Chuo cha Ualimu Shycom, Manispaa ya Shinyanga, likihusisha michezo mbalimbali na utoaji wa elimu.

Akizungumzia bonanza la PEPMIS 2024 Shinyanga, Meneja wa TANESCO Mkoa wa Shinyanga, Mhandisi Seraphine Lyimo amebainisha kuwa lengo la mfumo wa PEPMIS ni kuboresha uwajibikaji wa watumishi wa umma kupitia tathmini na ufuatiliaji wa majukumu yao.


"Tumepokea PEPMIS ili kutuwezesha kuchanganua malengo na kutathmini kazi zetu. Mfumo huu unahitaji mtumishi kuwa na cheki namba na namba ya siri, na unaweza kufanikisha yote haya kwa kutumia simu ya mkononi. Kila mtumishi anatakiwa kuingia kwenye mfumo na kujaza taarifa zake kwa ufanisi," amesema Mhandisi Lyimo.

Akitoa elimu ya matumizi ya mfumo wa PEPMIS, Mhandisi kutoka TANESCO Kanda ya Magharibi Mhandisi Felix Manuka amesisitiza umuhimu wa watumishi kutumia mfumo wa PEPMIS katika shughuli zao za kila siku ili kusaidia serikali kufuatilia maendeleo ya utekelezaji wa majukumu ya shirika.

Kwa upande wake, Kaimu Afisa Rasilimali Watu ambaye pia ni Makamu Mwenyekiti wa bonanza hilo, Robert Msemo, amewapongeza watumishi wa TANESCO kutoka wilaya zote tatu za mkoa wa Shinyanga kwa kujitokeza kwa wingi. huku , akisisitiza umuhimu wa mazoezi ya mwili kwa afya na kuongeza tija kazini.


Bonanza hilo, lililojulikana kama PEPMIS Bonanza 2024, limeambatana na michezo mbalimbali kama mbio za baiskeli, kukimbiza kuku, mchezo wa drafti, utambuzi wa vinywaji, kuokota machungwa, mbio za mita 200, kuvuta kamba, na mpira wa miguu.

Katika mchezo wa soka, timu ya TANESCO Shinyanga imeibuka mshindi kwa ushindi wa mabao 4-1 dhidi ya TANESCO Kahama na kuondoka na zawadi ya mbuzi.


Bonanza hili limeonesha si tu umuhimu wa mfumo wa PEPMIS, bali pia mshikamano na ushirikiano miongoni mwa watumishi wa TANESCO Mkoa wa Shinyanga.

Mhandisi kutoka Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) Kanda ya Magharibi 

Mhandisi Felix Manuka

 akizungumza wakati wa bonanza hilo.

Kaimu Afisa Rasilimali Watu ambaye pia ni Makamu Mwenyekiti wa bonanza hilo, Robert 

Msemo 

akizungumza wakati wa bonanza hilo. 

Meneja wa TANESCO Mkoa wa Shinyanga, Mhandisi Seraphine Lyimo

 akizungumza wakati wa bonanza hilo.

<<<<<<TAZAMA PICHA>>>>>




 

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com