Tundu Lissu, Mwenyekiti wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), ametangaza rasmi nia ya kugombea nafasi ya Uenyekiti wa Chama hicho katika uchaguzi ujao, nafasi ambayo kwa muda mrefu imekuwa ikishikiliwa na Freeman Mbowe.
Akizungumza na waandishi wa habari leo, Desemba 12, 2024, jijini Dar es Salaam, Lissu ameeleza kuwa kupitia nyadhifa mbalimbali alizopitia ndani ya chama, ameona maeneo ambayo yanahitaji mabadiliko na kuboreshwa.
Lissu amesema ameandika barua kwa Katibu Mkuu wa CHADEMA akiondoa kusudio la kugombea nafasi ya Makamu Mwenyekiti wa CHADEMA Bara na badala yake ameanzisha rasmi mchakato wa kugombea nafasi ya Uenyekiti wa Taifa.
Amesema anayo imani kwamba ana sifa za kutosha kugombea nafasi hiyo ya juu na kuiongoza CHADEMA kwa ufanisi, na kwamba wanachama wenzake wanapaswa kuwa na imani naye.
Aidha, Lissu amesisitiza kuwa wale wanaopinga au kuona ajabu uamuzi wake wa kugombea uenyekiti wangeweza kuwa hawajui au hawathamini urithi wa viongozi wa zamani kama Edwin Mtei na Bob Makani, ambao walikuwa na utamaduni wa kuachiana madaraka kupitia uchaguzi wa huru na wa haki.
Lissu ameongeza kuwa CHADEMA inahitaji mawazo mapya na uongozi mpya ili iweze kukua na kutimiza majukumu yake kwa ufanisi.
Social Plugin