Wabunge kadhaa wameripotiwa kujeruhiwa katika ajali iliyotokea maeneo ya Mbande Kongwa asubuhi ya leo Desemba 6, 2024 baada ya basi lililokuwa limebeba Wabunge kugongana na lori la mizigo.
Aidha, majeruhi wa ajali hiyo wamekimbizwa Hospitali ya Uhuru na Hospitali ya Benjamini Mkapa zilizopo mkoani Dodoma.
Kwa mujibu wa taarifa iliyochapishwa kwenye kurasa za Mitandao ya Bunge, Basi hilo lilikuwa limewabeba Wabunge wanaoelekea Mombasa, Kenya, kushiriki Mashindano ya 14 ya Mabunge ya Jumuiya ya Afrika Mashariki.
Social Plugin