Na Dotto Kwilasa,Dodoma
JESHI la Polisi Mkoa hapa limewatahadharisha wananchi kuachana na vitendo viovu katika msimu wa Sikukuu ya Krisimasi na mwaka mpya ikiwa ni pamoja na kujiepusha na upigaji wa fataki na baruti bila kibali kwa faida za usalama .
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Dodoma George Katabazi amebainisha hayo leo Desemba 23,2024 wakati akizungumza na waandishi wa habari kuhusu hali ya usalama mkoa wa Dodoma kuelekea sikukuu ambapo ameeleza kuwa kipindi hicho mara nyingi huambatana na matukio ya ajali,ugomvi na matukio mengine yasiyofaa kutokana na ulevi kupindukia.
Kamanda Katabazi amesema, “Kuna tabia ambayo inazuka wakati wa sherehe watu wanajisahau wanakunywa pombe kupitiliza matokeo yake wanasababisha kuingia katika hatari ya kusabisha ajali ambazo nizakujitakia na kuvamiwa,
Tunatoa rai kwa wananchi wote kusherekea sikukuu kwa amani na utulivu,kila mmoja ahakikishe anakunywa kwa kiasi na kwa wanaosafiri na madereva kuhakikisha wanaepuka matumizi ya vileo, "amesisitiza
Wakati huo huo Katabazi amesema katika operesheni waliyofanya wamekamata pikipiki 31 zinazozaniwa kuwa za wizi, bangi kilo 10, mirungi kilo 10, Tv, Radio na gari.
Amewalika wananchi kujitokeza kwa wingi kutambua mali hizo wakiwa na nyaraka halali.
“Tumefanikiwa kukamata kijana mmoja kati ya watatu waliokuwa wakisakwa na jeshi la polisi wakidhaniwa kuwa ni “panya road” Tunaendelea kusisitiza wananchi kutii sheria bila shuruti na kutoa ushirikiano kwa jeshi la polisi,”amesema
Social Plugin