Wananchi wa mtaa wa Sofi kata ya Mhongolo wakichimba mtaro ili kupunguza maji yanayotuama katika eneo hilo yanayosababisha kukatika kwa mawasiliano kati ya kata ya Mhongolo na kata ya Busoka Manispaa ya Kahama.
NA NEEMA NKUMBI -KAHAMA
Wakazi wa mtaa wa Sofi, Kata ya Mhongolo, Manispaa ya Kahama, wamechukua hatua ya kujitolea kufanya marekebisho ya barabara inayounganisha Sofi, Mhongolo na Busoka baada ya kukumbwa na changamoto ya mafuriko na ukosefu wa mawasiliano wakati wa masika.
Wananchi hao wameamua kuchangishana michango ya fedha na wengine kujitolea nguvu zao ili kuchimba mtaro na kununua mawe kwa lengo la kuepuka adha za mafuriko yanayozuia mawasiliano katika eneo hilo.
Mkazi wa Sofi, Neema Toyi, amesema kuwa barabara hiyo imekuwa kikwazo kikubwa kwao kila mwaka, hasa wakati wa masika, ambapo watoto wanashindwa kwenda shule na akina mama wajawazito wanapata ugumu wa kufika hospitali.
"Hii barabara inatutesa sana wakati wa mvua hata kama mvua haitanyesha katika mtaa wetu maji hutoka huko mjini na kutuvamia huku, tunapata shida sana watoto wanashindwa kuvuka kwenda shule, na ukinitazama mimi hapa na hali yangu(mjamzito) ninapata wasiwasi kama nikipata uchungu nitavukaje kwenda hospitali serikali na itutazame itujengee daraja hali ni mbaya sana", amesema Neema.
Beatus Mswati, mkazi mwingine, amekiri kwamba juhudi zao za kutengeneza barabara hiyo ni muhimu kwa ajili ya usalama wa familia zao na kuendelea na shughuli za kiuchumi.
Beatus amesema," Tumeamua kujitoa wenyewe kutengeneza barabara hii ili kuokoa maisha yetu na watoto wetu, tunapata shida wakati wa mvua tunashindwa kupitisha biashara zetu tutawezaje kulipa kodi? Maisha yetu ni magumu sana tunashindwa kukaa kwa amani kwa sababu ya maji yanayojaa hapa".
Mathias Mwita amesema kuwa licha ya juhudi za viongozi wakiwemo Diwani na Mbunge kutembelea eneo hilo, tatizo la barabara halijapata ufumbuzi wa kudumu hivyo, wananchi wameamua kujitolea kuungana na kuchangishana fedha ili kurekebisha barabara hiyo muhimu kwa maisha yao.
Mwenyekiti wa Mtaa wa Mhongolo, Emanuel Nangale, amepongeza juhudi za wananchi na kuongeza kuwa wamekuwa wakishirikiana na TARURA kuhakikisha barabara hiyo inapata bajeti.
"Sisi kama serikali ya mtaa tunatambua tatizo hilo eneo hilo ni korofi sana na tumepambana kuhakikisha barabara inapata bajeti na ikapata bajeti ya serikali kupitia TARURA, TARURA walikuja wakakwangua barabara ila hawajaweka changarawe na daraja ila tumewasiliana na Diwani wa Kata ya Mhongolo amesema analifuatilia kwa karibu", amesema Nangale.
Meneja wa TARURA Kahama, Joseph Mkwizu, amesema kuwa barabara hiyo ilikuwa na bajeti katika mwaka wa fedha 2023/2024 na kwamba Diwani ametoa maombi ya kipaumbele kwa eneo la Sofi katika bajeti ya mwaka 2025/2026 ili kutatua changamoto hiyo.
Mkwizu amefafanua, "Barabara hiyo inayounganisha Mhongolo Sofi na Busoka ilikuwa na bajeti katika mwaka wa fedha 2023/2024 ambapo tulijenga kalavati mbili, kuchoronga barabara km 4.7 na kuweka changarawe (moramu) km 1.3 katika eneo la Busoka iliyo gharimu shilingi milion 63.
Barabara inayounganisha Sofi na Mhongolo ni muhimu kwa usafiri wa wanafunzi wa shule ya msingi ya Bomani na Sekondari ya Nyashimbi, pamoja na wakazi wa eneo hilo katika shughuli zao za kilimo na biashara, Kukosekana kwa barabara hiyo kunaleta hasara kubwa kwao, na hivyo ni jambo la dharura kwa serikali kushughulikia tatizo hili kwa haraka.
Neema akielezea hali ngumu wanayokutana nayo wananchi wa mtaa wa Sofi kutokana na mvua, ambapo barabara inafurika maji kutoka mjini na Watoto wanashindwa kuvuka kwenda shule na hata wagonjwa, wakiwemo wajawazito kama Neema, wanapata shida kubwa kufika hospitali, huku akisisitiza kuwa serikali inapaswa kuchukua hatua ya dharura kuwajengea daraja ili kupunguza madhila haya.

Meneja wa TARURA Kahama, Joseph Mkwizu, akielezea juhudi za kuboresha barabara inayounganisha Mhongolo Sofi na Busoka.
Mathias Mwita akielezea juhudi za viongozi kama Diwani na Mbunge kutembelea eneo hili, lakini tatizo la barabara halijapata ufumbuzi wa kudumu.
Wananchi wa mtaa wa Sofi wakichimba mtaro ili kupunguza maji yanayotuama katika eneo hilo yanayosababisha kukatika kwa mawasiliano kati ya kata ya Mhongolo na kata ya Busoka

Social Plugin