Na Mariam Kagenda _Kagera
Mkuu wa wilaya ya Karagwe Kalanga Lisser amedhibitisha kutokea kwa ajali katika eneo la Kihanga wilayani humo.
Dc Kalanga wakati akizungumza na malunde blog Kagera amesema kuwa kwa sasa hawezi dhibitisha vifo ni vingapi na majeruhi ila ajali ni mbaya.
Amesema kuwa roli likiwa limebeba maparachichi limeigonga kwa nyuma Haice iliyokuwa ikitokea wilaya ya Karagwe kwenda bukoba na Haice kugonga Costa iliyokuwa ikitoka Bukoba kwenda Karagwe.
Mmoja wa mashuhuda amesema kuwa ameweza kusaidia kutoa baadhi ya maiti katika gari .