Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Mhe. Dkt. Doto Biteko amesema Bara la Afrika lina zaidi ya watu milioni 600 ambao bado hawajafikiwa na nishati ya umeme hivyo rasilimali zilizopo zitumike kubadilisha maisha ya watu ikiwemo katika sekta ya umeme.
Dkt. Biteko ameyasema hayo Desemba 04, 2024 wakati akifunga Mkutano wa Pili wa Mwaka wa Jumuiya ya Wahasibu Wakuu wa Nchi za Afrika (AAAG) Jijini Arusha.
Amesisitiza rasilimali zilizopo barani Afrika zitumike kubadilisha hali za maisha ya watu ili ziweze kuleta tija.
Social Plugin