Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

WATUMISHI TUUMIE MTEJA ANAPOKOSA HUDUMA: MHANDISI BWIRE



Kaimu Afisa Mtendaji Mkuu wa Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Dar es salaam (DAWASA), Mhandisi Mkama Bwire amewaasa watumishi wa Mamlaka kua na desturi ya kuwasikiliza na kutatua changamoto za wateja kwa wakati ili kuboresha huduma inayotolewa na Mamlaka na kamwe wasizoee changamoto za wateja na kuchukulia kawaida.

Mhandisi Bwire ameyasema hayo katika siku ya pili ya kikao kazi na Watumishi wa Mikoa ya kihuduma DAWASA Kawe, Ilala, Kinondoni, Magomeni na Makongo.

"Nawaomba watumishi wote tukawe wepesi katika kutatua changamoto za wateja na kuwasikiliza, hii itasaidia zaidi kuboresha mahusiano na mawasiliano baina ya Taasisi na wateja wake, wote tuumie tunapoonaa mteja anakosa huduma ya maji" ameeleza Mhandisi Bwire.

Bwire ameongeza kuwa ni jukumu la kila mtumishi ndani ya Mamlaka kuhakisha wateja wanaohudumiwa na DAWASA katika Mkoa wa Dar es salaam na Pwani wanapata huduma ya majiasafi.

Mhandisi Bwire amewasihi menejimenti katika mikoa ya kihuduma kufanya kazi kwa ukaribu na viongozi wa vyama vya wafanyakazi Ili kuhakikisha watumishi wanafanya kazi katika mazingira Bora na wezeshi katika kutimiza Majukumu yao ya kila siku.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com