Na Dotto Kwilasa,DODOMA...
Kaimu Katibu Mkuu Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Xavier Daudi amesema Ofisi hiyo inatarajia kufanya kikao kazi cha Mwaka cha Wakuu wa Idara za Utawala na Usimamizi wa Rasilimaliwatu katika Wizara, Sekretarieti za Mikoa, Mamlaka za Serikali za Mitaa, Idara zinazojitegemea, Taasisi, Mashirika ya Umma na Wakala za Serikali kuanzia Desember 17 hadi 19 mwaka huu.
Amesema kikao kazi hicho kitaongozwa na Kaulimbiu isemayo "Kusimamia Sera na Sheria za Utumishi wa Umma kupitia Mifumo ya Usimamizi wa Rasilimaliwatu na Utawala ya Kidijitali iliyoboreshwa” na Mgeni Rasmi wakati wa Ufunguzi anatarajiwa kuwa Waziri wa Nchi - Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Mhe. George Simbachawene.
Kauli hiyo ameitoa Desembar 12,2024 jijini Dodoma wakati akizungumza na waandishi wa habari kwenye Ofisi za Wizara hiyo ambapo amewataka Wakuu wote wa Idara za Utawala na Usimamizi wa Rasilimaliwatu,
Kujisajili kwenye mfumo wa https://tsms.gov.go.tz ili kushiriki kikao hicho na kwamba mwisho wa kujisajili ni tarehe 13 Desemba, 2024.
Kutokana na umuhimu wa kikao kazi hicho amewataka Waajiri wote nchini kuwaruhusu Wakuu hao wa Idara kushiriki kikamilifu katika kikao kazi hicho ili kujifunza mbinu mbalimbali za kutoa huduma bora kwa wananchi na kupunguza malalamiko.
"Nitoe rai kwa wahusika wote wa kikao hicho cha Desember 17 hadi 19 wafike katika Ukumbi wa Mikutano wa Jiji la Dodoma uliopo katika Mji wa Serikali Mtumba tarehe 16 Disemba, 2024 kuanzia saa 10:00 Jioni ili kuchukua vitambulisho na makabrasha kabla ya kuanza kikao , "amesema
Ametaja malengo kikao kazi hicho kuwa ni kubadilishana uzoefu katika masuala mbalimbali ya Usimamizi wa Rasilimaliwatu na ukumbushana masuala mbalimbali yanayohusu Usimamizi wa Rasilimaliwatu katika Utumishi wa Umma ikiwemo matumizi ya mifumo ya kidijitali ya e-Watumishi, e-Uhamisho, e-Utendaji, e-Mrejesho, HR Assessment.
Lengo lingine ni kupeana maelekezo kuhusu masuala mbalimbali yanayohusu Usimamizi wa Rasilimaliwatu katika utumishi umma kwa kuzingatia Shabaha na vipaumbele vya Taifa.
"Tunafanya hayo yote ili kuwahudumia wananchi kwa ufanisi hivyo tumeona ni vyema zaidi kutoa hiyo nafasi ili watumishi wa Umma waweze kujifunza zaidi matumizi ya mifumo mipya ya TEHAMA kwa lengo la kuwafikia wananchi kwa ukaribu," amefafanua.
Sambamba na hayo Mkurugenzi huyu ameeleza kuwa Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora (OR-MUUUB) ina majukumu mbalimbali kwa mujibu wa Hati ya Mgawanyo wa Majukumu kwa Mawaziri kama ilivyotangazwa katika Gazeti la Serikali Toleo Na. 619A & 619B la tarehe 30/8/2023 na kwamba moja ya majukumu hayo ni kusimamia Rasilimaliwatu katika Utumishi wa Umma na Utawala wa Utumishi wa Umma.
Kwa upande wake Mkurugenzi wa Utawala wa Utumishi wa Umma Felister Shuli amesema Rasilimaliwatu ni nguzo ya Uendelezaji wa rasilimali zingine hivyo ni muhimu kujengewa uelewa.
Kwa upande wake, Mkurugenzi wa Utawala wa Utumishi wa Umma, Felister Shuli, amesema Rasilimaliwatu ni nguzo ya Uendelezaji wa rasilimali nyingine, hivyo ni muhimu kujengewa uelewa.
Amesisitiza kuwa ufanisi wa Taasisi hutegemea uwezo na maarifa ya wafanyakazi wake na kuongeza kuwa uwepo wa mifumo bora ya usimamizi wa rasilimaliwatu kutasaidia kuboresha utendaji kazi, kupunguza urasimu, na kuongeza ubora wa huduma kwa wananchi.
Naye Mkurugenzi wa Usimamizi wa Rasilimaliwatu SACP Ibrahim Mahumi amesema
Serikali itaendelea kuweka mikakati ya kuboresha mafunzo na maendeleo ya wafanyakazi ili kufikia malengo ya maendeleo endelevu na kueleza kuwa licha ya kuwepo kwa baadhi ya changamoto kikao kazi hicho kitatoa nafasi ya kuzijadili na kuzipatia ufumbuzi.
Social Plugin