WIZARA YA KATIBA NA SHERIA, GIZ WAWAKUTANISHA WATAALAMU WA JINSIA KUPITIA MWONGOZO WA KUPAMBANA NA UKATILI WA KIJINSIA


NA EMMANUEL MBATILO, DAR ES SALAAM

SERIKALI ya Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia Wizara ya Katiba na Sheria wamewakutanisha kwa kushirikiana na Shirika la Maendeleo la Ujerumani GIZ wamewakutanisha wataalamu mbalimbali wa masuala ya jinsia kwa lengo la kupitia mwongozo wakufundishia wasaidizi wa kisheria ili kuwasaidia kukabiliana na changamoto za ukatili wa kijinsia.

Akizungumza leo Disemba 02,2024 Jijini Dar es Salaam,wakati wa ufunguzi wa mkutano huo Wakili wa Serikali, Athumani Msosore amesema mwongozo huo unatarajiwa kupunguza vitendo vya ukatili wa kijinsia kwa kuwasaidia wasaidizi wa kisheria kuwa na wazo la pamoja bila kutofautiana.

Amesema mwongozo huo umekusudiwa kuanza kufanya kazi katika ngazi za chini kwenye Serikali za Mtaa na Vijiji kwani wenyeviti pamoja na watendaji wao hushughulika na kesi hizo kwa sababu wapo karibu na Jamii.

Pamoja na hayo Msosore amesema Wizara imekuwa na desturi ya kutoa mafunzo kwenye makundi maalumu pamoja na shule mbalimbali ili mtu anapotendewa ukatili ajue wapi pakwenda kuripoti tukio hilo kwa lengo la kuchukua hatua za kisheria.

Kwa upande wake,Mratibu wa huduma ya msaada wa Kisheria Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM) Emmanuel Baruti ameeleza kuwa wanatamani kuwa na mwongozo ambao utatumika katika mazingira tofautitofauti ili ulete matokeo chanya.

Amesema kuwa kutokana na suala la ukatili kuhussisha taasisi nyingi ambapo kila taasisi inautaratibu wake wakaona vyema msaidizi kisheria apate mwongozo ambao utamsadia kuzitatua changamoto hizo.

Nae Afisa Magereza Hamis Kituli amesema mwongozo huo umekusudia kujenga uelewa wa pamoja ambapo utasaidia kufundishia katika maeneo tofauti ofauti bila kutofautiana kwenye uelewa wa suala hilo.

Vilevile, Wakili wa Shirika la WILDAF, Zakia Msangi ameeleza kuwa mwongozo huo umekusudia kusaidia wahanga wa ukatili wa kijinsia kwani wanapotendewa vitendo vya kikatili wanatarajia kuona wanapokwenda kwa wasaidizi wa kisheria wanapata msaada pamoja na ushauri kwa kuzingatia usiri.

Mkutano huo umejumuisha wataalamu mbalimbali wanaohusiana na masuala ya ulinzi wa haki za wanawake na watoto.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com
Previous Post Next Post