Na Kadama Malunde - Malunde 1 blog
Jumla ya vyandarua 1,542,836 vyenye dawa vinatarajiwa kusambazwa mkoani Shinyanga mwezi huu, ikiwa ni sehemu ya juhudi za Serikali na wadau wake kupambana na ugonjwa wa malaria.
Akizungumza leo Januari 6, 2025, wakati wa kikao kazi cha Waandishi wa Habari Mkoa wa Shinyanga kuhusu kampeni ya ugawaji vyandarua vyenye dawa, Afisa Mwandamizi kutoka Wizara ya Afya, Peter Gitanya, ameeleza kuwa vyandarua hivyo vitasambazwa bure kwa kila kaya, kupitia ushirikiano wa Serikali na wadau wa afya.
Amesema Vyandarua hivi vitasambazwa kwa wananchi wa Shinyanga kupitia Wizara ya Afya , mpango wa Taifa wa Kudhibiti Malaria (NMCP) kwa kushirikiana na OR- TAMISEMI, Bohari ya Dawa (MSD) na Wadau wa afya lengo kuu ni kupunguza maambukizi ya malaria.
Ameongeza kuwa kampeni hii ni sehemu ya mkakati wa kitaifa wa kupambana na malaria, na inatarajiwa kuwa na mchango mkubwa katika kupunguza vifo vinavyosababishwa na ugonjwa huo.
Gitanya amesisitiza kuwa vyandarua vyenye dawa ni mojawapo ya njia bora za kudhibiti maambukizi ya malaria, kwani vinasaidia kuua mbu wanaosambaza vijidudu vya ugonjwa huu.
Amesema usambazaji wa vyandarua utachangia kupunguza vifo na maambukizi, hasa katika mikoa inayokumbwa na changamoto kubwa ya malaria kama vile Shinyanga.
“Mkoa wa Shinyanga utapata vyandarua vyenye dawa milioni 1.5, ambapo kila kaya itapata vyandarua kulingana na idadi ya watu. Kwa kila kaya, chandarua kimoja kitagawiwa kwa watu wawili,” amesema Gitanya.
Amesisitiza kwamba, kaya ambazo hazitaandikishwa kwa ajili ya kupokea vyandarua haziwezi kupewa vyandarua, hivyo amehimiza wananchi kushiriki kikamilifu katika zoezi la uandikishaji linaloendelea hadi Januari 15, 2025.
Zoezi la uandikishaji kaya linaendelea katika mkoa wa Shinyanga, ambapo wananchi wanapewa kadi maalumu ya usajili ili kupokea vyandarua wakati wa usambazaji utakaofanyika kuanzia Januari 16, 2025. Serikali imeweka wazi kwamba usambazaji utafanyika kwa usawa, na wananchi wote wa maeneo ya vijijini pia watafikiwa.
Gitanya pia ameeleza kwamba, kwa mwananchi ambaye atapoteza kadi yake ya usajili, ataweza kupata chandarua chake kwa kwenda kwenye kituo husika, kwani taarifa za kila kaya zitakuwa zimehifadhiwa.
Gitanya amezungumzia hali ya malaria nchini na kusema kuwa mkoa wa Shinyanga ni miongoni mwa mikoa yenye kiwango cha juu cha malaria, ukiwa ni asilimia 16, huku kiwango cha kitaifa kikiwa ni asilimia 8.
Ameongeza kwamba mikoa mingine kama vile Tabora, Mtwara, na Kagera pia ina viwango vikubwa vya malaria, na Serikali inaendelea na jitihada za kupunguza maambukizi katika maeneo haya kwa kutumia mbinu mbalimbali, ikiwa ni pamoja na ugawaji wa vyandarua vyenye dawa.
Mchango wa Vyombo vya Habari
Katika kikao hicho, waandishi wa habari wamehusishwa kikamilifu katika kuhamasisha jamii kuhusu matumizi sahihi ya vyandarua vyenye dawa.
Kaimu Mganga Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga, Faustine Mlyutu, ameipongeza Serikali kwa kuanzisha kampeni hii, na akawahimiza waandishi wa habari kuelimisha jamii kuhusu umuhimu wa kutumia vyandarua vya dawa kwa usahihi, ili kupambana na malaria.
“Waandishi wa habari, tumieni kalamu zenu kuelimisha jamii kuhusu matumizi sahihi ya vyandarua vyenye dawa. Hii ni vita dhidi ya malaria, na mkoa wa Shinyanga unahitaji msaada wenu ili kufikia lengo la kuwa na jamii isiyo na malaria,” amesema Mlyutu.
Naye Mwenyekiti wa Klabu ya Waandishi wa Habari Mkoa wa Shinyanga, Greyson Kakuru, amesema kuwa waandishi wa habari watatumia fursa hii kutoa elimu kwa umma kuhusu matumizi sahihi ya vyandarua vyenye dawa, na kuhakikisha kuwa ujumbe wa kupambana na malaria unafika kwa kila mwananchi.
Kwa ujumla, Serikali inazidi kutoa mchango mkubwa katika kupambana na malaria nchini Tanzania, na kampeni hii ya ugawaji vyandarua vyenye dawa ni hatua muhimu katika kutokomeza ugonjwa huu ifikapo mwaka 2030.
Wananchi wanahimizwa kushiriki kikamilifu katika zoezi la uandikishaji na matumizi sahihi ya vyandarua vya dawa, ili kuleta mabadiliko chanya katika kupambana na malaria.
Afisa Mwandamizi kutoka Wizara ya Afya Peter Gitanya kupitia Mpango wa Taifa wa Kudhibiti Malaria (NMCP) akiwasilisha mada kwenye kikao kazi hicho.
Afisa Mwandamizi kutoka Wizara ya Afya Peter Gitanya kupitia Mpango wa Taifa wa Kudhibiti Malaria (NMCP) akiwasilisha mada kwenye kikao kazi hicho.
Afisa Mwandamizi kutoka Wizara ya Afya Peter Gitanya kupitia Mpango wa Taifa wa Kudhibiti Malaria (NMCP) akiwasilisha mada kwenye kikao kazi hicho.
Kaimu Mganga Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Faustine Mlyutu akizungumza kwenye kikao kazi hicho.
Afisa kutoka TAMISEM Best Yoram akizunguma kwenye kikao kazi hicho.
Afisa mradiwa Malaria kutoka Wizara ya Afya Wilfred Mwafongo akizungumza kwenye kikao kazi hicho.
Mwenyekiti wa Klabu ya waandishi wa habari Mkoa wa Shinyanga Greyson Kakuru akizungumza kwenye kikao kazi hicho.
Mratibu wa Malaria Mkoa wa Shinyanga Betty Shayo akizungumza kwenye kikao kazi hicho.
Mratibu wa elimu ya afya kwa umma Moses Mwita akizungumza kwenye kikao kazi hicho.
Afisa kutoka Wizara ya Afya Atley Kuni akiwasilisha mada kwenye kikao kazi hicho.
Afisa kutoka Wizara ya Afya Atley Kuni akiwasilisha mada kwenye kikao kazi hicho.
Afisa kutoka Wizara ya Afya Atley Kuni akiwasilisha mada kwenye kikao kazi hicho.
Afisa kutoka Wizara ya Afya Happiness Nania akiwasilisha mada.
Afisa kutoka Wizara ya Afya Happiness Nania akiwasilisha mada.
Afisa kutoka Wizara ya Afya Happiness Nania akiwasilisha mada.
Mwenyekiti wa Jamii inayopambana na Malaria Tanzania (CONAMET), Gesonko Paul akizungumza kwenye kikao hicho
Social Plugin