Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

MATIKO CUP YAZINDULIWA KWA KISHINDO, MAMILIONI YA FEDHA KUTOLEWA


Mbunge wa viti maalumu Esther Matiko
Mkuu wa wilaya Tarime Meja Edward Gowele

Na Helena Magabe Tarime.
Mbunge wa viti maalumu Esther Matiko ameweka historia na kuvunja rekodi ya kutumia zaidi ya milioni 85 kwenye kuzindua Matiko cup kitendo kilichowaacha midomo wazi mashabiki wa michezo walioshuhudia uzinduzi huo pamoja na viongozi mbalimbali.

Katika uzinduzi huo uliofanyika katika uwanja wa mpira wa  shamba la bibi Tarime mjini na kuzinduliwa na Mgeni rasmi Mkuu wa wilaya Tarime Meja Edward Gowele amempongeza Mhe. Matiko kwa hatua hiyo kubwa ya Matiko Foundation kuzindua Matiko cup kwani michezo ni afya,ajira na starehe.

Ametumia fursa hiyo  kuwaomba wadau mbalimbali kujitokeza kumwunga mkono Esther Matiko kupitia na kuiomba serikali kuwaunga mkono wale wote wanaonzisha michezo kwani kupitia michezo Vijana wanakuwa busy  na michezo na kusaidia kupunguza uharifu,pia ni ajira na burudani kwa Watazamaji.

Naye mdau wa michezo, Jackson Kagonye amempongeza Mhe.  Matiko kwa hatua hiyo na kusema kuwa kuanzisha michezo si  jambo rahisi hata yeye aliwahi kufikiria  kuanzisha lakini  akashindwa naye Mjumbe wa mkutano mkuu Taifa Chochorio Daniel amepongeza hatua hiyo na kusema kuwa pesa zilizotumika katika uzinduzi huo ni sawa na pensheni ya kustaafu huku akiahidi kuchangia milioni 3 kumuunga mkono Mhe Matiko.

Hata hivyo Mhe. Matiko ameahidi zawadi mbalimbali kwa washindi katika fainali ambapo mshindi  kwanza atapata milioni 15,mshindi  wa  pili medali ya fedha na shilingi milioni 10,mshindi wa tatu medali ya Shaba na shilingi milioni 5 na mshindi wa nne atapata milioni 2.

 Vile vile Mchezaji bora atapata kiatu cha dhahabu na shilingi laki 2,kipa bora atapata groves ya dhahabu na shilingi laki 2,timu bora itapata laki 5 pamoja na kipa bora atapata shilingi laki 5.

Aidha katika uzinduzi huo imefanyika michezo mbali mbali mingi huku zikitolewa zawadi   zikiwemo jezi  kwa  timu 20   kwaaji ya kuanza mechi Januari 4 katika viwanja mbali mbali vya mipira vipatavyo 10 huku akitoa nyavu za magori na vifaa kwa watu wa huduma ya kwanza.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com