Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

Breaking : TAZAMA HAPA MATOKEO YA MTIHANI WA KIDATO CHA NNE (CSEE) 2024

Bofya Hapa kutazama matokeo



Baraza la Mitihani la Tanzania (NECTA) limetangaza matokeo ya Kidato cha Nne kwa mwaka 2024, ambapo watahiniwa 477,262 kati ya wanafunzi 516,695 wenye matokeo wamefaulu kwa kupata madaraja ya I, II, III na IV.

NECTA imesema ufaulu huo umepanda kwa asilimia 3, hivyo kufikia asilimia 92.37 kutoka asilimia 89.36 mwaka 2023.

Kwa mwaka 2024, takwimu zinaonesha idadi ya watahiniwa waliopata madaraja ya I, II na III imeongezeka na kufikia 221,953 sawa na asilimia 43, ikilinganishwa na mwaka 2023 ambapo idadi ilikuwa  197,426 sawa na asilimia 37.4.

Idadi ya watahiniwa waliopata daraja la IV na zero imepungua, hivyo ubora wa ufaulu umepanda kwa asilimia 5.6.

Pia limewafutia matokeo ya Kidato cha nne wanafunzi 67, waliogundulika kufanya udanganyifu pamoja na watano kwa kuandika matusi kwenye majibu ya mtihani waliofanya wa kuhitimu Elimu ya sekondari.

Aidha Baraza limezuia matokeo ya wanafunzi 459 kwa sababu za kiafya zilizopelekea kushindwa kufanya mtihani wa Kidato cha nne 2024


Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com