Na Marco Maduhu & Kadama Malunde - Shinyanga Serikali mkoani Shinyanga imeadhimisha kumbukumbu ya kuzaliwa kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kupanda miti 500 katika Shule ya Msingi Mapinduzi, Manispaa ya Shinyanga.
Tukio hili limefanyika leo, Januari 27, 2025, ikiwa ni siku ya kuzaliwa kwa Rais Samia, ambaye alizaliwa mwaka 1960, na hivyo kufikisha umri wa miaka 65.
Katika kuendeleza jitihada za serikali za utunzaji wa mazingira, Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga, Mhe. Anamringi Macha, ameongoza kampeni hii ya upandaji miti.
Akizungumza wakati wa tukio hilo, Macha amesema kwamba mkoa wa Shinyanga umeamua kupanda miti 500 katika shule hiyo kama sehemu ya kusherehekea siku ya kuzaliwa kwa Rais Samia, lakini pia ni sehemu ya kutekeleza maelekezo yake kuhusu utunzaji wa mazingira na kukabiliana na mabadiliko ya tabia nchi.
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Anamringi Macha akizungumza wakati akiongoza Kampeni ya Upandaji Miti ili kuunga mkono jitihada za serikali za utunzaji wa mazingira na kusherehekea kumbukumbu ya kuzaliwa kwa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan
“Miti hii 500 tumeipanda leo, siku ya kumbukumbu ya kuzaliwa kwa Rais wetu Dkt. Samia Suluhu Hassan. Kupanda miti ni heshima kubwa kwa Rais wetu na ni moja ya hatua muhimu katika kuhakikisha mazingira yetu yanatunzwa. Naagiza miti hii itunzwe na ikue vizuri, ili siku tukija hapa tuone mazingira yanavyokuwa,” amesema Macha.
Aidha, Macha amesisitiza kuwa wananchi, taasisi na halmashauri za mkoa wa Shinyanga wanapaswa kuendelea na kampeni ya kupanda miti katika maeneo yao.
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga, Mhe. Anamringi Macha, akimwagia maji mti katika Shule ya Msingi Mapinduzi, Manispaa ya Shinyanga
Amewataka wafugaji na wananchi wanaochunga mifugo katika maeneo yaliyopandwa miti kuchukuliwa hatua kali ikiwa watabainika kuvunja sheria za utunzaji wa mazingira.
Amesema ,"Mti mmoja ukikatwa, ipandwe miti zaidi ya miwili," na kuonya dhidi ya tabia ya kukata miti kiholela bila kibali cha mamlaka husika.
Katika hatua nyingine, Macha ametoa pongezi kwa Rais Samia kutokana na utendaji wake mzuri, akitolea mfano Mkutano Mkuu wa Masuala ya Nishati uliofanyika Tanzania na kuwakutanisha viongozi kutoka nchi mbalimbali.
Amesema matumizi ya nishati safi ya kupikia ni muhimu, kwani yanaweza kupunguza utegemezi wa mkaa, ambao unachangia uharibifu mkubwa wa mazingira.
Mkuu wa Wilaya ya Shinyanga, Julius Mtatiro, ameonyesha dhamira ya kuendeleza kampeni ya kupanda miti, huku akihakikisha kuwa miti 500 iliyopandwa itafuatiliwa na itatunzwa.
Meya wa Manispaa ya Shinyanga, Elias Masumbuko, ameeleza kuwa maelekezo yote aliyotoa Mkuu wa Mkoa yatatekelezwa, na pia wataendelea kuhamasisha wananchi na halmashauri kujiunga na kampeni hii ya kupanda miti.
Wanafunzi wa Shule ya Msingi Mapinduzi, ambao wamehusika katika zoezi la kupanda miti, wameonesha furaha yao na kuelezea umuhimu wa kupanda miti.
Mwanafunzi Godfrey Mgeta ameelezea jinsi walivyofahamu umuhimu wa miti,na ameahidi kuwa mabalozi wazuri wa kuhamasisha familia zao na jamii kuendelea kupanda miti katika maeneo yao.
Zoezi hili limemalizika kwa kumuimbia Rais Samia wimbo wa “Happy Birthday,” kama ishara ya heshima na upendo kutoka kwa wananchi wa Shinyanga.
Sherehe za kumbukumbu ya kuzaliwa kwa Rais Samia Suluhu Hassan katika Mkoa wa Shinyanga ni mfano mzuri wa jinsi jamii inavyoshirikiana na serikali katika kudumisha mazingira bora na kuhamasisha utunzaji wa rasilimali za taifa.
Kupanda miti si tu ni hatua ya kupambana na mabadiliko ya tabia nchi, bali pia ni ishara ya uzalendo na dhamira ya dhati ya kuendelea kulinda dunia yetu kwa vizazi vijavyo.
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Anamringi Macha akizungumza wakati akiongoza Kampeni ya Upandaji Miti ili kuunga mkono jitihada za serikali za utunzaji wa mazingira na kusherehekea kumbukumbu ya kuzaliwa kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kupanda miti 500 katika Shule ya Msingi Mapinduzi, Manispaa ya Shinyanga.
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Anamringi Macha (katikati) akiwa ameshikilia mti wakati akiongoza Kampeni ya Upandaji Miti ili kuunga mkono jitihada za serikali za utunzaji wa mazingira na kusherehekea kumbukumbu ya kuzaliwa kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kupanda miti 500 katika Shule ya Msingi Mapinduzi, Manispaa ya Shinyanga.
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Anamringi Macha akiandaa mti tayari kwa kuupanda katika Shule ya Msingi Mapinduzi, Manispaa ya Shinyanga ikiwa ni sehemu ya Kampeni ya Upandaji Miti ili kuunga mkono jitihada za serikali za utunzaji wa mazingira na kusherehekea kumbukumbu ya kuzaliwa kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Anamringi Macha akipanda mti katika Shule ya Msingi Mapinduzi, Manispaa ya Shinyanga ikiwa ni sehemu ya Kampeni ya Upandaji Miti ili kuunga mkono jitihada za serikali za utunzaji wa mazingira na kusherehekea kumbukumbu ya kuzaliwa kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga, Mhe. Anamringi Macha, akimwagia maji mti katika Shule ya Msingi Mapinduzi, Manispaa ya Shinyanga, kama sehemu ya Kampeni ya Upandaji Miti, kuunga mkono jitihada za serikali za utunzaji wa mazingira na kusherehekea kumbukumbu ya kuzaliwa kwa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan
Mwanafunzi wa shule ya msingi Mapinduzi Manispaa ya Shinyanga akizungumza wakati Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga, Mhe. Anamringi Macha akiongoza kampeni ya Kampeni ya Upandaji Miti, kuunga mkono jitihada za serikali za utunzaji wa mazingira na kusherehekea kumbukumbu ya kuzaliwa kwa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan

Mkuu wa Wilaya ya Shinyanga Mhe. Wakili Julius Mtatiro akipanda mti katika Shule ya Msingi Mapinduzi, Manispaa ya Shinyanga ikiwa ni sehemu ya Kampeni ya Upandaji Miti ili kuunga mkono jitihada za serikali za utunzaji wa mazingira na kusherehekea kumbukumbu ya kuzaliwa kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan

Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Anamringi Macha akigawa miti wakati akiongoza Kampeni ya Upandaji Miti ili kuunga mkono jitihada za serikali za utunzaji wa mazingira na kusherehekea kumbukumbu ya kuzaliwa kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan.
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Anamringi Macha akigawa miti wakati akiongoza Kampeni ya Upandaji Miti ili kuunga mkono jitihada za serikali za utunzaji wa mazingira na kusherehekea kumbukumbu ya kuzaliwa kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan.
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Anamringi Macha akigawa miti wakati akiongoza Kampeni ya Upandaji Miti ili kuunga mkono jitihada za serikali za utunzaji wa mazingira na kusherehekea kumbukumbu ya kuzaliwa kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan.
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Anamringi Macha akizungumza wakati akiongoza Kampeni ya Upandaji Miti ili kuunga mkono jitihada za serikali za utunzaji wa mazingira na kusherehekea kumbukumbu ya kuzaliwa kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kupanda miti 500 katika Shule ya Msingi Mapinduzi, Manispaa ya Shinyanga.
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Anamringi Macha akizungumza wakati akiongoza Kampeni ya Upandaji Miti ili kuunga mkono jitihada za serikali za utunzaji wa mazingira na kusherehekea kumbukumbu ya kuzaliwa kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan
Mkuu wa Wilaya ya Shinyanga Mhe. Julius Mtatiro akizungumza wakati wa Kampeni ya Upandaji Miti ili kuunga mkono jitihada za serikali za utunzaji wa mazingira na kusherehekea kumbukumbu ya kuzaliwa kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan

Meya wa Manispaa ya Shinyanga Mhe. Elias Ramadhan Masumbuko akizungumza wakati wa Kampeni ya Upandaji Miti ili kuunga mkono jitihada za serikali za utunzaji wa mazingira na kusherehekea kumbukumbu ya kuzaliwa kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan
Social Plugin