Na Mwandishi wetu - Malunde 1 blog Dar es salaam
Hatua hiyo inakuja baada Vituo 10 vya Watoto yatima kupewa msaada wa vyakula na vifaa mbalimbali vya shule kutoka Kampuni ya Sino Truck.
Akitoa msaada huo Meneja Mkazi wa Kampuni hiyo ya Sino Truck,Li Zhang Yuan amesema wamefanya hivyo kama ishara ya kuonyesha upendo kwa watoto hao.
Amesema bidhaa hizo walizotoa ni kuonyesha jinsi wanavyojali watoto hao.
"Tunaweka ndoto yetu kwenye mioyo yao, ili wakumbuke Sino Truck inawajali," amesema.
Akiwakilisha vituo hivyo 10 vilivyopokea msaada huo, Meneja wa Kituo cha Long quantity Children Care, Jane Shao amesema jambo hilo lililofanywa kwa watoto hao ni sehemu ya kujaliwa.
" Tunashukuru Kampuni ya Sino Truck kwa kuwatambua watoto wetu. Tunaomba waendelee kushirikiana ili watoto hawa watimize ndoto zao," amesema.
Ameelezea changamoto zinazokabili watoto hao kuwa ni shule na upungufu wa chakula.hivyo anaomba wadau wengine waweze kuwapatia msaada ili watoto hao wapate viwango bora katika malazi, chakula. Michezo na mengineyo.
Vituo vilivyopatiwa msaada ni Nira, Kind Heart, Udo, Hiyari A, Hiyari B, Longquan, Chamazi na Umra.
Social Plugin