Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

HAYA NDIYO MAMBO YATAKAYOIBEBA CCM UCHAGUZI 2025

                      

John Francis Haule

Katiba ya nchi yetu inasisitiza kuwa viongozi wa ngazi ya Urais, ubunge, na udiwani wanapaswa kuchaguliwa kila baada ya miaka mitano. 

Tangu kuanzishwa kwa mfumo wa vyama vingi mnamo 1995, kumeshuhudiwa ushindani mkali wa sera na maono kati ya vyama pamoja na viongozi wa vyama husika. 

Sheria ya vyama vingi ya 1992 iliwezesha usajili wa vyama vingi vya siasa, ikiwa ni pamoja na NCCR-Mageuzi, CUF, CDM, na vingine vingi, wakiwemo ACT-Wazalendo. Vyama hivi vyote vinapata ithibati sawa kwa mujibu wa sheria za vyama vya siasa.

Hali ya CCM Tangu Asili yake

Chama Cha Mapinduzi (CCM) kilipoasisiwa mwaka 1977, kimeendelea kushika dola kwa ridhaa ya wananchi, kutokana na sera, imani, na misingi yake ya kihistoria, ikiwa ni pamoja na falsafa ya ukombozi wa binadamu kutoka katika hali ya unyonge na kuheshimu utu wa binadamu.

Madhumuni ya CCM

Kama ilivyo kwa chama chochote cha kisiasa, madhumuni ya CCM ni kushinda uchaguzi na kushika dola. Chama hiki, kikiwa na misingi imara ya kulinda maslahi ya wananchi, kimeweza kustahimili changamoto za mfumo wa vyama vingi tangu ulipoanza na kuendelea kubaki madarakani kwa imani ya wananchi.

Vyama vingi vya Afrika vilivyoongoza mapambano ya ukombozi vimekumbana na changamoto za kutofuata matakwa ya wananchi au kupoteza imani. Hata hivyo, CCM imedumu kwa kujenga misingi imara ya kulinda maslahi ya wananchi, na hii ndiyo sababu ya kuendelea kuwa chama cha kuaminika hadi leo.

Ushindi wa CCM katika Uchaguzi wa Serikali za Mitaa 2024

Katika uchaguzi wa serikali za mitaa wa 2024, CCM imeshinda kwa asilimia 99%, jambo linalothibitisha kuwa wananchi bado wana imani na chama hiki. Ushindi huu unathibitisha kuwa vyama vingine havina mizizi imara katika ngazi za mashina, na badala yake vimejikita kutoa tuhuma mitandaoni.

Misingi ya Ushindi wa CCM 2025

CCM ina nguvu kubwa ya kushinda uchaguzi wa 2025 kutokana na mambo yafuatayo:

  1. Idadi ya Wana-Chama na Wafuasi wake
    Kwa sasa, CCM ina zaidi ya milioni 19 za wanachama, na idadi hii inaendelea kuongezeka. Hii ni mtaji mkubwa kwa CCM kwani vyama vingine havina theluthi ya wafuasi hawa, na hivyo ushindi wa CCM 2025 ni uhakika wa asilimia 100%.

  2. Mtandao wa Mabalozi na Wajumbe wa CCM
    CCM ina mfumo wa mabalozi na wajumbe hadi ngazi za mashina, ambao ni muhimu katika kujenga mizizi ya chama na kuhakikisha wanachama wanashiriki katika kupiga kura. Huu ni mtaji wa kipekee kwa ushindi wa CCM.

  3. Demokrasia ya Ndani ya Chama
    CCM ina mfumo imara wa kubadilishana madaraka, ambapo viongozi wanachaguliwa kwa njia za haki. Hii inaifanya CCM kuwa chama cha kuaminika, tofauti na vyama vingine vinavyokumbwa na changamoto za uongozi.

  4. Falsafa ya R4 za Rais Samia
    Falsafa ya maridhiano, ustahimilivu, kuboresha, na kujenga upya imejenga imani kubwa kwa CCM. Rais Samia amethibitisha kuwa kiongozi madhubuti na imara, akiongoza kwa weledi mkubwa.

  5. Huduma za Kijamii na Miundombinu
    CCM imefanikiwa kutoa huduma bora za kijamii, ikiwa ni pamoja na huduma za afya na msaada wa kisheria kupitia Samia Legal Aid. Programu za afya na elimu pia zimeimarika, na miradi ya kimkakati kama SGR na umeme wa Nyerere imeongeza uaminifu kwa chama.

  6. Usalama na Ulinzi
    CCM imedumisha hali ya usalama na amani, jambo ambalo limesaidia wananchi kufanya shughuli zao za kimaisha bila hofu. Hii inathibitisha ufanisi wa vyombo vya ulinzi na usalama chini ya uongozi wa CCM.

  7. Diplomasia ya Kimataifa
    Serikali ya CCM imeimarisha diplomasia ya kiuchumi, na Tanzania sasa inaongoza katika biashara za EAC, kama ilivyosemwa na Rais William Ruto wa Kenya. Hii inathibitisha nguvu ya CCM katika uwanja wa diplomasia.

Hitimisho

Kwa jumla, CCM inayo turufu nyingi za ushindi katika uchaguzi wa 2025, ikiwa ni pamoja na uimara wake wa kimfumo, uongozi imara, huduma bora kwa wananchi, na mifumo ya usalama na diplomasia. Vyama pinzani vimekosa umoja na umadhubuti, jambo linalowafaidi CCM. Hivyo, ushindi wa CCM 2025 ni wa uhakika.



Makala hii imeandikwa na

John Francis Haule

Mkuu  wa Soko Kuu  la  Arusha

(Market master)

Simu 0756717987 au 0711993907


Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com