Mtoto huyo ameugua ugonjwa huu tangu akiwa na miezi sita, na mpaka sasa hali yake inazidi kuwa mbaya.
Dorcas anasema mtoto wake amekuwa akihangaika na maumivu makali ya mgongo kwa miaka mingi, hali inayomfanya kushindwa kutembea au kukaa, na muda mwingi analia kwa uchungu.
"Mtoto wangu amekuwa akiteseka sana. Hasa hivi anatumia dawa za mshipa ili kupunguza maumivu, lakini hali yake inaendelea kuwa mbaya, na kwa sasa dawa hizi zimeisha na hana pesa ya kuzinunua" anasema Dorcas kwa huzuni akizungumza na Malunde 1 blog.
Bima ya Afya Yasitishwa
Mtoto Angel alipata matibabu kupitia bima ya afya ya NHIF ambayo ilimsaidia kupata huduma muhimu katika Hospitali ya CCRBT Msasani Jijini Dar es salaam.
Hata hivyo, bima hiyo ilisitishwa mwaka 2023, na kwa sasa Dorcas ameshindwa kumudu gharama za matibabu kwa sababu ya ukosefu wa fedha na baba wa mtoto alimtelekeza baada ya mtoto kupata changamoto hizo za kiafya.
"Mwanzo alikuwa akipata matibabu kupitia NHIF, lakini sasa sina tena bima hiyo kwa sababu ilisitishwa na hali yangu kifedha ni ngumu. Hivi sasa, siwezi kumudu kwenda hospitali kama nilivyokuwa nikienda hapo awali, na mtoto wangu anahitaji msaada wa haraka," Dorcas anaongeza.
Hali Inavyoendelea
Kwa sasa, mtoto Angel anashindwa kutembea, kukaa na kujihudumia mwenyewe, anategemea msaada wa mama yake ambaye anambeba kila wakati kwa sababu hawezi kusimama wala kutembea.
Dorcas anasema, "Natembea na mtoto wangu kila mahali kwa sababu hawezi kutembea mwenyewe. Maumivu yanazidi kila siku."
Dorcas pia ameeleza kwamba anajishughulisha na ujasiriamali wa kuuza sabuni za maji ili kujikimu kimaisha, lakini hawezi kumudu gharama kubwa za matibabu kwa mtoto wake.
Ombi la Msaada
Dorcas anawaomba Watanzania , wadau wa afya na watu wote wenye mapenzi mema kujitolea kumsaidia mtoto wake apate matibabu ya haraka.
Anahitaji msaada wa kifedha ili kugharamia matibabu, na pia anahitaji msaada wa kupata kiti maalum kwa ajili ya mtoto wake ili kumrahisishia maisha yake ya kila siku.
Msaada Unaohitajika:
- Matibabu ya haraka ya UTI wa Mgongo kwa mtoto Angel.
- Msaada wa kifedha kwa ajili ya matibabu na huduma za afya.
- Kiti maalum cha mtoto (wheelchair) ili kumrahisishia harakati.
Wasiliana na Dorcas
Kwa yeyote anayetaka kutoa msaada, tafadhali wasiliana na Dorcas kupitia namba ya simu:
0696204320 (Airtel Money - Jina: Kibibi Issa).
Msaada wa haraka utasaidia kuokoa maisha ya mtoto Angel na kumrudisha kwenye hali ya afya njema.
Dorcas anaamini kwamba kwa pamoja, watanzania na watu wema wataleta mabadiliko makubwa kwa mtoto huyu aliye katika hali ngumu.
Social Plugin