Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

BWERANYANGE KARAGWE WAJA NA WAZO LA KUANZISHA SEMINARI YA WASICHANA


Mkuu wa Shule ya Wasichana Bweranyange Rehema James Mkoha akizungumza na waandishi wa habari

Na Lydia Lugakila - Karagwe.

Shule ya Wasichana Bweranyange iliyopo katika kata ya Nyabiyoza Wilayani Karagwe Mkoani Kagera imeamua kuja na wazo la kuwa na Seminari ya wasichana huku matarajio yao makubwa yakiwa ni kuitengeneza shule hiyo katika viwango vya hali ya juu kiseminari na kumjenga mtoto wa kike kiroho kimwli na kiakili.

Kauli hiyo imetolewa na mkuu wa shule ya Wasichana Bweranyange Rehema James Mkoha Januari 10,2025 wakati akizungumza na waandishi wa habari juu ya masuala mbalimbali yahusuyo elimu shule hapo.

Rehema alisema kuwa shule hiyo inayomilikiwa na kanisa la kiinjili ya kilutheri Tanzania KKKT Dayosisi ya Karagwe inayoongozwa na Askofu Benson Bagonza ilianzishwa mwaka 2007 ina kidato cha kwanza hadi cha nne inatarajia kuanzisha Seminari ya wasichana ili mtoto wa kike anapotoka shuleni hapo hata akionekana kuanzia tembea yake watu waseme kweli anatokea shule ya kanisa na shule ya dini ambayo inatengeneza maadili.

"Tunataraji kumtengeneza mtoto wa kike ili aonekane wa Seminari kweli kweli tutawatengeza mtoto wetu ikiwa ni kazi ambayo tunaendelea nayo shuleni hapa" alisema Bi Rehema.

Aliongeza kuwa wazazi wa watoto hao waishio maeneo ya shule na mbali na shule hiyo wamekuwa wakitoa shuhuda zao na kushangaa mabadiliko ya muda mfupi kwa watoto wao ki nidhamu, maadili na kuwa wanapokuwa nyumbani wakati wa rikizo wamekuwa ni watoto wa kukaa ndani kufanya kazi za darasani pamoja na usafi.

Mkuu huyo wa shule hiyo alisema wataendeleza kuwafundisha watoto hao maisha yao ya nidhamu binafsi wala sio nidhamu ya woga.

"Seminari tunayotarajia ni ya kumnoa mtoto wa kike avutie kwani ndiye Mama wa kesho, tunataka awe Mama bora na kizazi chake kiwe bora kwa baadae", alisema Mkoha.

Aliongeza kuwa shule hiyo inaendeshwa kwa mfumo wa amali unaolenga watoto kujitegemea wanapomaliza shule ili wawe na uwezo wa kujiajiri au kuajiriwa.

Aliongeza kuwa mkondo wa amali ulianzishwa mwaka 2024 shuleni hapo baada ya Serikali kutangaza kwamba inatengeneza mkondo huo wenye lengo la kumtengeneza mtoto kuwa na maarifa bora hivyo na wao wanawafundisha watoto kilimo, kutunza wanyama, Afya za wanyama na kutengeneza mazao pamoja na kazi nyingine zitakazowasaidia mbeleni kwani ni faida sana kuona mtoto anatoka na ujuzi wa kujitegemea ikiwemo mapishi na ushonaji.

Aidha alipongeza walimu wa shule hiyo kwa matokeo mazuri ya mtihani wa kidato cha kwanza 2024/2024 kwani yametoka yakiwa na nguvu ya aina yake ambapo wanafunzi waliofanya mtihani huo wa Taifa walikuwa 12 ambapo Daraja la kwanza ni wanafunzi 5, Daraja la pili ni 4 na watatu ni 3 na kuwa wamejipanga kwa Mwaka huu wa 2025 kuwapokea watoto wote hata wenye udhaifu ili wawanoe na kuwapiga msasa wa kiroho kimwili na kiakili ambapo amewakumbusha wazazi wenye kipato cha kati, kizuri na kidogo kuwapeleka watoto shule ili kuvuna maarifa.

Hata hivyo kwa upande wa wazazi wa watoto hao akiwemo Asimwe Jonas Emmanuel Murokozi kutoka kata ya Nyabiyoza walikiri shule hiyo kuwa bora katika masuala ya kitaaluma nidhamu na dini kwani haibagui dini katika kutoa elimu ambapo amewaomba wazazi kujitahidi kuwapeleka watoto shuleni hapo ili kuwa na Taifa bora kwa sasa na baadaye

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com