Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

CHARLES GEORGE WAITARA KUZIKWA KESHO ,AWALIZA WANANCHI KWA ALAMA ALIYOIACHA TARIME



Na Helena Magabe,Tarime.

Mwili wa Charles George Waitara utazikwa kesho Januari 17,2025 nyumbani kwao Bomani wilayani Tarime mkoani Mara.

Baba mdogo wa marehemu Charles ,Mwalimu Amos Waitara amesema Charles atakumbukwa kwa upendo na ucheshi wake watu wote ambaye alipenda Tarime kuliko kitu chochote.

"Charles alikuwa na upendo wa hali ya juu na ucheshi alipenda Tarime kuliko kitu chochote alikuwa anasema Tarime ndio kwetu na ndio maana alianza kuekeza Tarime anekufa kabla hajatimiza ndoto yake kwa hiyo tuangalia namna ya kumuenzi ", amesema Amos.

Rafiki wa karibu wa Marehemu Charles ,James Sengwa amesema Marehemu alikuwa mcheshi ,mwenye upendo kwa kila mtu aliyeheshimu watu wa kila lika hali aliyomfanya kuwa na marafiki wengi hadi waliomzidi umri.

Charles George Waitara alizaliwa Aprili 30,1985 na kufariki dunia Januari 12,2025 katika hosptali ya Taifa ya Muhimbili baada ya kuugua kwa muda mrefu takribani miaka mitano.
Marehemu Charles George Waitara enzi za uhai wake alikuwa Mwanasheria kitaaluma ambaye atakumbukwa na wana Tarime kwa alama aliyoiacha katika Hospitali ya Bomani Tarime.

Ikimbukwe kwamba Oktoba 1, 2019 Marehemu Charles alitoa msaada wa vifaa viwili vya maabara Biochemistry pamoja microbiologia , kompyuta za10 na magodoro 180 enzi hizo wagonjwa katika hosptali hiyo walikuwa wanalala zaidi ya mgonjwa mmoja katika kitanda kimoja .

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com