Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

ASSUMPTER AAHIDI KUENDELEZA USHIRIKIANO KATIKA KUTOA ELIMU KWA VICOBA ILI KUVINUFAISHA ZAIDI

Na Lydia Lugakila - Bukoba.

Kauli hiyo imetolewa na aliyewahi kuwa  Mbunge wa Jimbo la Nkenge Mhe. Assumpter Mshama alipokuwa akiongea na waandishi wa habari Kagera hivi karibuni  katika uzinduzi wa siku ya Ijuka Omuka.

Amewahimiza Watunza fedha za vikundi Mkoani humo wakiwemo Wana Misenyi juu ya kuwa waaminifu katika masuala ya  fedha za ili kunufaika zaidi badala ya kujutia walichowekeza huku akitaka akina mama wapate furaha na fedha zao na sio majonzi.

Bi, Assumpter amesema baadhi ya  wananchi wamekuwa wakijinyima kwa kuchanga fedha kupitia vikundi mbali mbali hivyo watunza fedha wanatakiwa kuwa waaminifu ili kila mmoja apate alichowekeza baada ya kufikia wakati wa kugawana

Aidha Bi Assumpter amesema ataendelea kuwapatia ushirikiano wa kutosha na yupo tayari kuendelea kutoa elimu kuhusu vikundi hivyo (Vicoba) ili kila mtu anufaike kadili anavyokuwa amewekeza.

Ikumbukwe kuwa Mhe. Assumpter alikuja na kauli mbiu ya "Umaskini sio fungu langu" wakati akiomba ridhaa ya kuwa mbunge wa Jimbo la Nkenge huku akihamasisha Wananchi wa Jimbo la Nkenge hasa wanawake kuwekeza pesa (Vicoba) kwa ajili ya maendeleo yao binafsi.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com