Katika hotuba yake, Kanali Ahmed alisema tukio hilo limemsikitisha sana, kwani limepoteza nguvu kazi ya taifa, wakiwemo walimu muhimu katika jamii. Alitoa wito kwa vyombo vya usalama barabarani kuongeza juhudi za ukaguzi wa vyombo vya moto na kutoa elimu ya mara kwa mara ili kuepuka ajali kama hizo.
Viongozi wa chama na serikali walihudhuria kwenye tukio la kuaga miili hiyo na walitoa salamu za pole kwa familia za marehemu.
Marehemu waliotambulika katika ajali hiyo ni: Vicent Alel Milinga (Dereva),Damas Damasi Nambombe (Mwalimu),Judith Joseph Nyoni (Mwalimu),John Silvester Mtuhi (Mwalimu) ,Dominic Abeat Ndau (Mwalimu) naBoniface Bosco Mapunda (Raia)
Social Plugin