Na Mapuli Kitina Misalaba
Jeshi la Polisi Mkoa wa Shinyanga limefanikiwa kuwakamata watuhumiwa wawili wa mauaji ya dereva aliyefahamika kwa jina la Lazaro, mwenye umri wa miaka 35, ambaye mwili wake ulikutwa ndani ya shimo la choo katika kata ya Lubaga, Januari 18, 2025.
Kwa mujibu wa taarifa zilizotolewa na Kamanda wa
Polisi Mkoa wa Shinyanga, Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi Janeth Magomi, Lazaro aliuawa kwa kupigwa na kitu kizito kichwani kabla ya mwili wake
kutupwa shimoni.
“Kabla
ya tukio hilo kuna mfanyabiashara anaitwa Yona alifungua kesi ya wizi wa kuaminiwa
Januari 16, 2025 dhidi ya huyo aliyekuwa dereva wake ambaye kwa sasa ni
marehemu, mlalamikaji alieleza kuwa dereva wake hamuoni na pia gari lake
halionekani tangu Januari 14 kwahiyo alizileta hizi taarifa kwetu na ufuatiliaji
wa jeshi la polisi ulianza mara moja, ambapo Januari 17, 2025 tulifanikiwa
kukamata watuhumiwa wawili wakiwa na gari hilo aina ya Toyota Hiace wakiwa
wanajaribu kuvuka mpaka kwenda nchini Kenya katika eneo la Tarimelorya”.
amesema Kamanda Magomi.
Jeshi la Polisi limefanikiwa kuwakamata watuhumiwa
wawili Januari 17, 2025, wakiwa na gari hilo wakijaribu kuvuka mpaka kuelekea
Kenya katika eneo la Tarimelorya. “Tunaendelea na upelelezi wa kina na pindi
utakapokamilika, jalada litapelekwa kwa Mwanasheria wa Serikali kwa hatua zaidi
za kisheria,” amesema SACP Magomi.
Kamanda Magomi amelaani vikali kitendo cha mauaji
hayo akisema, “Ni kosa kisheria kujichukulia sheria mkononi. Kila mtu ana haki
ya kuishi, na sisi Jeshi la Polisi tutahakikisha elimu inatolewa kwa wananchi
ili kupunguza makosa ya jinai, hasa mauaji.”
Social Plugin