Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

MKUU WA MKOA WA RUVUMA ATOA WITO WA KUIMARISHA ELIMU KATIKA MUHULA MPYA WA MASOMO 2025




Na Regina Ndumbaro - Ruvuma 

Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma, Kanali Ahmed Abbas Ahmed, amewataka wazazi  na wananchi kuhakikisha wanafunzi wanaripoti shule mapema ili kuanza masomo. 


Amewahimiza kutatua changamoto za msingi kama sare za shule na madaftari, akisisitiza kuwa elimu ni haki ya kila mtoto. 


Aidha amewataka wadau wanaohusika na kuboresha miundombinu ya shule kukamilisha kazi zao haraka na kwa viwango bora ili kuepuka kuchelewesha maendeleo ya sekta ya elimu.


Kanal  Ahmed Abbas pia ametembelea shule za sekondari za Songea girls na Mfaranyaki  kuangalia maendeleo ya shule hizo ambazo zipo katika halmashauri ya Wilaya ya songea Mkoani Ruvuma na kuonana na walimu wa shule hizo.

 Ametoa wito kwa walimu kuhakikisha wanatimiza wajibu wao kwa kujituma na kuwahamasisha wanafunzi kufikia malengo yao ya kielimu. 


Ameongeza kuwa kila shule inapaswa kupanda miti ya matunda na mboga mboga ili kuboresha mazingira ya shule na kuchangia lishe bora. 

Pia amemtaka Katibu Tawala wa Mkoa kusimamia kikamilifu maendeleo ya sekta ya elimu na kuhakikisha kila mdau anatimiza jukumu lake ipasavyo kwa manufaa ya jamii nzima.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com