Na Mwandishi wetu.
Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM) kimepongeza ushirikiano wa kitaaluma uliopo baina ya Tanzania na China ambao umeendelea kuchochea wanafunzi kutoka nchi hizo kujifunza lugha za Kiswahili na Kichina.
Pongezi hizo zimetolewa jijini Dar es Salaam kwenye ukumbi wa Maktaba ya chuo hicho Katika kuadhimisha Mwaka Mpya wa ‘Spring festival’ na Naibu Makamu Mkuu wa Chuo (UDSM) - Taaluma, Prof. Bonaventure Rutinwa , ambapo amesema ongezeko la wanafunzi wanaojifunza lugha hizo ni alama ya mafanikio ya ushirikiano huo.
Naye Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Urafiki wa Tanzaniana China Joseph Kahama amesema kuwa Tanzania na china wataendelea kushirikiana katika elimuili kukuza lugha lakini kupanua wigo wa biashara.
Kwa upande wake mwakilishi wa Balozi wa China hapa nchini, Tanzania Che Zhaguang amesema shirika la Umoja wa Mataifa (UN)wametambua sasa kuwa kiswahili ni lugha rasmi ambapo ni mafanikio makubwa kwa nchi Ndiyo maana urafiki baina ya china na Tanzania utaendelea kuwa imara.
Social Plugin