Na Barnabas kisengi Dodoma
Chama cha Mapinduzi kata ya kilimani Jijini Dodoma kimefanya mafunzo ya uongozi na maadidi kwa viongozi wake wote wanaoshiriki mkutano mkuu wa kata ya Kilimani.
Lengo la mafunzo hayo ni kuwajengea uwezo wa kufahamu Juu ya uongozi na maadidi katika nafasi zao mbalimbali walizo nazo
Awali akifungua mafunzo hayo mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi wilaya ya Dodoma Charles Mamba amesema mafunzo hayo ni muhimu kwao kwakuwa kila moja atatambua wajibu wake katika nafasi aliyonayo ya uongozi katika ngazi ya kata, tawi,shina na kwa wenyeviti wa mitaa na wajumbe wao.
Mkufunzi wa mafunzo hayo Comredi Samweli Ikwabe amesema mafunzo ya uongozi na maadidi ni muhimu sana kwa viongozi hao wa chama cha Mapinduzi na wenyeviti wa Serikali za mitaa na wajumbe wao waliochaguliwa No ember 27 mwaka jana kwakuwa yamekuja wakati muafaka.
Ikwabe amesema kumekuwa na tofauti mara nyingi katika nafasi zao kwakuwa wengi woa walikuwa hawajui mipaka ya nafasi zao za uongozi
"Sasa natumaini kila moja amepata kitu hapa baada ya kupata mafunzo haya ya uongozi na maadidi naamini sasa yatakuwa chachu katika utendaji wa majukumu ya kazi zeno mtakazokuwa mkizifanya kwa kuwahudumia wanachama na wananchi wote katika ngazi Mbalimbali katika maeneo yenu ya utendaji wa kazi zenu za kila siku"amesema Ikwabe
Awali akiwakaribisha wajumbe wa mkutano mkuu wa kata ya kilimani Jijini Dodoma mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi kata ya kilimani Comredi Nathan Chibeye amesema yeye kama mwenyekiti alishirikiana na kamati ya siasa ya kata ya kilimani kuanda mafunzo hayo ya siku moja ya uongozi na maadidi kwa vwajumbe wa mkutano mkuu wa kata ya kilimani
Comredi Chibeye amesema wao kama chama cha Mapinduzi kata ya kilimani waliona ni vema kuwapatia viongozi wao mafunzo ili kuweza kuwajengea uwezo viongozi hao kujua juu ya uongozi na maadidi ili ikawarahisishie katika utendaji wa majukumu yao ya kila siku
Mafunzo hayo yamefanyika katika ukumbi wa Balozi Lusinde uliopo katika kata ya kilimani Jijini Dodoma.
Social Plugin