Na Helena Magabe - Tarime
Akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake amesema kitendo cha mbunge huyo kuchochea wananchi kudai katiba mpya akiwa kwenye sherehe aliyoalikwa na moja ya mtia nia ,akihoji kwanini Mbunge hakufika na kudai kuwa hakuna maendeleo Tarime ,hakuna barabara za lami ni kitendo ambacho kimemkera na ni uvunjifu wa sheria za nchi.
Amesema Mbunge huyo anatakiwa kufanya maendeleo Nchini kwake hasa kwenye Jimbo lake ambalo yeye si mgeni anazijua barabara za jimboni kwake zilivyo mbovu hasa njia ya Kehancha ambayo ilijengwa zaidi ya miaka ishirini iliyopita hakuna maendeleo aliyofanya na Jimboni kwake ni Mbunge Bubu ambaye haongelei Jimbo lake na hayuko kwenye rekodi ya vyombo vya habari .
Akiendelea kuzungumza amesema Katiba mpya sio kipaumbele cha wananchi wa Tarime bali wananchi wanahitaji maendeleo kama vile ,maji,umeme elimi,afya barabara na mahitaji muhimu hiyo katiba mpya anayowahamasisha wadai haitawasaidia kwani hata huko jimboni kwake katiba haijaleta majibu ya changamoto zinazowakabili wananchi wake hivyo aache kuzungumzia vitu ambavyo haviingii akilini.
Ameiomba Serikali ya Kenya kumchukulia hatua mbunge huyo kwa sababu nchi ya Kenya ni jirani na ndugu hivyo asingependa kuona anasababisha mgogoro wa kudai katiba na kusababisha uvunjifu wa amani baina ya nchi mbili ambazo zina mahusiano mazuri.
" Kwanza sisi utamaduni wetu ni tofauti na wa nchi yao sisi tuna heshima si rahisi kutukana Kiongozi Kila mtanzania ana wajibu wa kuilinda heshima ya Nchi yake kule kwao wanatukana viongozi kwanza kura wanapiga kwa ukabila,huku sisi tunafata sifa asilete mambo yake ya kisiasa every day nikutia kauli ambazo hazina tija "alisema Kembaki.
Aidha amesema hakuna mtia nia ayemnyima usingizi kwani maendeleo amefanya na wananchi wanamkubali na katika sekta zote amezitendea haki kwa upande wa barabara ambayo alisema Bomani hakuna lami amesema itapata lami karibia maeneo yote na kwamba mbali na kilometa 6 za lami zilizo kwenye mpango zimeongezwa nyingine 18 ambapo kata ya Nyamisangura na Bomani zitapewa kipaumbele.
Social Plugin