Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

KIBAKWE WAKABIDHIWA GARI LA WAGONJWA



Na Barnabas kisengi, Mpwapwa

Zikiwa takribani siku 42 zimepita tangu ulipofanyika Uchaguzi wa Viongozi wa serikali za mitaa kwa nafasi za wenyeviti wa Serikali za mitaa,vijiji na vitongoji hapa nchini Novembar 27 2024,wananchi  wa Kata ya Mtera wamefanikiwa kukabidhiwa gari la kubebea wagonjwa katika kata ya mtera Jimbo la kibakwe wilayani mpwapwa

Akikabidhi gari hilo Mhe Waziri wa nchi Ofisi ya Rais menejment ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora na Mbunge wa Jimbo la Kibakwe George Simbachawene mbele ya viongozi na wananchi wa kata ya mtera January 7 2025 amesisitiza kulitunza gari hilo ili liweze kuwa msaada kwa wananchi hao hasa akina mama wajawazito ambao wengi wamekuwa wakipoteza maisha kwa kutoweza kukimbizwa haraka katika kituo Cha afya kwaajili ya kupewa huduma ya kujifungua.

Waziri Simbachawene amesema gari hilo litakuwa mkombozi mkubwa kwa wananchi wa mtera kwa kuwapatia huduma wagonjwa wote.

Kwaupende wake Diwani wa Kata ya mtera Jimbo la kibakwe Mhe Robert Maulya amemshukuru serikali ya awamu ya sita na Mbunge wao kwa kuwasikiliza na kiwaokoa shida yao waliyokuwa nayo muda mrefu katika kituo Chao cha afya kwa kukosa gari la kubebea wagonjwa

Diwani Maulya amesema serikali ya awamu ya sita imeweza kuisikia kero yao na kuzitatua .

Diwani huyo amesema kuwa yeye kama mwakilishi wa wananchi katika kata ya mtera atahakikisha wanalitunza gari hilo ambalo sasa ni mkombozi katika kituo cha afya cha mtera.

Mkulugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya wilaya ya Mpwapwa Bi Mwanahamisi Ally amesema kuwa gari hilo limekuja mahususi kufanya kazi katika kituo hicho cha afya cha mtera

"Niwasisitize viongozi wa kata ya mtera na wananchi wote hapa kuwa gari hili limekuja kwaajili yenu na kufanya kazi za kutoa huduma kwa wagonjwa wote hivyo litumike kwa shughuli zilizopangwa na sii vinginevyo sitasita kuchukua hatua pindi nikisikia gari hili linatumika vibaya.

Mkulugenzi Mwanahamisi amesema serikali ya awamu ya sita imayoongozwa na RAIS WETU Dr SAMIA SULLU HASSAN imeamua kujikita katika sekta ya afya kuhakikisha inaokoa vifo vya wakina mama wajawazito hivyo sasa hili gari ni mkombozi kwenu litumieni vizuri naemlitunze.

Wananchi wa kata ya mtera wameishukuru serikali ya awamu ya sita kwa kuwajali kwa kuwapatia gari ambalo kwao ni mkombozi wa kata ya mtera na vijiji vya jirani.








Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com