Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

MBUNGE WA SOLWA AHMED SALUM AKABIDHI GARI LA WAGONJWA LYABUKANDE


Mbunge wa Jimbo la Solwa Mkoani Shinyanga Mh. Ahmed Salum kushoto akikata utepe wakati akikabidhi gari la kubeba wagonjwa (AMBULANCE) katika kituo cha afya tarajiwa Lyabukande katika halmashauri ya Wilaya ya Shinyanga leo January 08, 2025.
**
Mbunge wa Jimbo la Solwa Mkoani Shinyanga Mhe. Ahmed Salum amekabidhi gari la Wagonjwa katika Kituo cha afya tarajali cha Lyabukande halmashauri ya Wilaya ya Shinanga leo January 8, 2025 ikiwa ni moja ya mahiataji makubwa kwa wananchi wa kata hiyo.

Akikabidhi gari hilo litakalotumika kusafirisha wagonjwa wakiwemo wajawazito waliokuwa wakipata kadhia na changamoto wakati wa kujifungua kutumia gharama kubwa za kukodi magari binafsi ambao alichangia wengi wao kujifungulia njiani na wengine kupoteza maisha.

Amesema kuwa upatikanaji wa gari hilo ni moja ya maombi aliyowasilisha kwa serikali kupitia Makamu wa Rais Dkt. Philip Mpango alipofanya ziara ya kikazi Moani Shinyanga kwa kusema kuwa moja ya ameneo yenye idaidi kubwa ya watu ni Kata za Lyabukande, Mwakitolyo na Didia ambazo zinahiatji huduma za vituo vya afya na gari za kubeba wagonjwa.

Mh. Ahmed amesema kuwa licha ya eneo hilo kuwa zahanati lakini limekuwa likitoa huduma zenye hadhi ya kituo cha afa kutokana na kuhudumia wananchi wa kata zaidi ya tatu pamoja na wakazi kutoka wilaya jirani zinazozunguka eneo hilo.

Aidha amesema kuwa tayari Serikali imekwisha peleka fedha kiasi cha Shilingi milioni 666.6 kwa ajili ya ujenzi wa kituo caha fya Lyabukande kitakachokuwa kinatoa huduma karibu kwa wananchi waliokuwa wakitumia kati ya laki 2, 3 hadi 5 kukodi magari a watu binafsi kwenda katika hospitali ya halmashauri, na ile ya Rufaa

Wakati huo huo amekabidhi pikipiki kwa ajili ya utaoji wa huduma za chanjo kwa wananchi wa kata hiyo ili watoto wao waweze kupewa chanjo katika mandhari walioko pasi kusafiri umbali mrefu kufusta hudma za chanjo.

Mganga Mkuu wa halmashauri ya Shinyanga Dkt. Nuru Yunge amesema kuwa wanayo hospitali moja ya halmashauri, vituo vya afya vitano na zahanati,44 ambazo zinasaidia kutoa huduma kwa wakakzi wa halmashauri hiyo ambapo kituo cha afya kimoja na zahanati 5 zinatoka mashirika binafsi.

Dkt. Yunge amesema kwa mwaka wa fedha 2024/2025 wataarajia kufungua zahanati 7 kutoka katika vijiji vya Nyang’ombe, Songambele, Manyada, Kizungu, Mwamalulu, Mwandutu na Nyida ikiwa ni mkakakti wa serikali wa kusogeza karibu hduuma za afya karibu na wananchi wa ameneo husika

Aidha amesema katika fedha zilizoteolewa na serikali katika uejnzi wa kituo cha afya Lyabukande jumla ya shughuli 8 zianatarajiwa kufanyika ikiwa ni Pamoja na Jengo la Wagonjw wa Nje,(OPD), Maabara, Jengo la Upasuaji, jengo la kufulia,ukamilishaji wodi ya wazazi,ukamilishaji choo cha nje, mfumo wa maji safi na Mfumo wa umeme vitakavyosaidia kutolewa kwa huduma hiyo

Naye mwenyekiti wa halmashauri ya Shinyanga Ngassa Mboje amempongeza Mbunge Ahmed Salum kwa kuhakikisha anasimamia suala la upatikanji wa huduma bora za afya kwa wananchi wake ambapo amekuwa mmoja wa watetezi wa wananchi katika jimbo hilo

Ngassa amewataka wasimamizi wa Gari na pikipiki zilizokabidhiwa leo kuahkikisha wanasimamia na kutekeleza wajibu wao ipasavyo kwa kutoa huduma bira kwa wananchi kwani walikumbana na kadhia kubwa ikiwemo gahrama kubw az akukodi kwa watu binafsi

Nao baadhi ya wakazi wa Lyabukande akiwemo Rahel Paulo, Marry Maige na Darusi Bukenda wameishukuru Serikali ya awamu ya sita kwa kuwapatia gari hilo ambalo lilmekuwa msaada mkubwa kwa jamii hiyo kwa kuwa kina mama wngi walipoteza watoto na wengine kufariki kwa kukosa usafiri wa uhakika na haraka sanjali na kutumia gahrama kubwa kukodi magari ya watu binafsi.
Mbunge wa Jimbo la Solwa Mkoani Shinyanga Mh. Ahmed Salum kushoto akikabidhi ufunguo wa gari la kubeba wagonjwa(AMBULANCE) katika kituo cha afya tarajiwa Lyabukande katika halmashauri ya Wilaya ya Shinyanga leo January 08, 2025.
mwenyekiti wa halmashauri ya Shinyanga Ngassa Mboje akizungumza kabla ya kukabidhi gari la wagonjwa Lyabukande
Mganga Mkuu wa halmashauri ya Shinyanga Dkt.Nuru Yunge akisoma hali ya utaoji wa huduma za afya katika halmashairi ya Shinyanga kabla ya kukabidhiwa gari la kubeba wagonjwa katika kituo cha afya Tajrajiwa Lyabukande







Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com