Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

OFISI YA WAKILI MKUU WA SERIKALI YASHIRIKI MAADHIMISHO YA WIKI YA SHERIA DODOMA 2025

Naibu Wakili Mkuu wa Serikali, Bi. Alice Mtulo akisaini kitabu cha wageni baada ya kuwasili kwenye banda la Ofisi ya Wakili Mkuu wa Serikali wakati ya Maadhimisho ya Wiki ya Sheria yaliyoanza leo Jijini Dodoma.
Rais Mstaafu wa Awamu ya Nne wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akizungumza na watumishi na wadau wa Mahakama ya Tanzania wakati akizindua  Maadhimisho ya Wiki ya Sheria yaliyoanza leo Jijini Dodoma.
Jaji Mkuu wa Tanzania, Mhe. Prof. Hamis Juma akitoa salamu za Mahakama kwa watumishi na wadau wa Mahakama wakati wa uzinduzi wa Maadhimisho ya Wiki ya Sheria yaliyoanza leo Jijini Dodoma.
Watumishi wa Ofisi ya Wakili Mkuu wa Serikali wakishiriki maandamano ya Wiki ya Sheria kabla ya uzinduzi wa maadhimisho hayo yanayoendelea Jijini Dodoma.
Rais Mstaafu wa Awamu ya Nne wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akimsalimia Jaji Mkuu wa Tanzania, Mhe. Prof. Hamisi Juma baada ya kuwasili kwenye viwanja vya Kituo Jumishi cha Mahakama Kuu kwa ajili ya kushiriki maandamano ya uzinduzi wa Wiki ya Sheria Jijini Dodoma.
Rais Mstaafu wa Awamu ya Nne wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akimsikiliza Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Usimamizi wa Mashauri na Udhibiti Ubora, ndugu Camilius Ruhinda alipotembelea banda la maonesho la Ofisi ya Wakili Mkuu wa Serikali wakati wa uzinduzi wa Maadhimisho ya Wiki ya Sheria Jijini Dodoma.
Watumishi wa Ofisi ya Wakili Mkuu wa Serikali wakiwa ndani ya banda la maonesho la Ofisi hiyo kwa ajili ya kutoa elimu ya msaada wa kisheria kwa wananchi na wadau watakaotembelea banda hilo wakati wa maadhimisho ya Wiki ya Sheria yanayoendelea Jijini Dodoma.
Rais Mstaafu wa Awamu ya Nne wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akiwa na Viongozi wa Mahakama na Taasisi za Sekta ya Sheria baada ya kuzindua Maadhimisho ya Wiki ya Sheria yanayofanyika Jijini Dodoma.
Watumishi wa Ofisi ya Wakili Mkuu wa Serikali, Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali na Mahakama wakimsikiliza Rais wa Awamu ya Nne wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Jakaya Mrisho kikwete wakati wa Uzinduzi wa Maadhimisho ya Wiki ya Sheria yaliyofanyika leo Jijini Dodoma.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com