Na Mwandishi Wetu, KIGOMA.
Waziri wa Uchukuzi Prof. wa kiwanja cha Ndege Kigoma kufanya kazi usiku na mchana ili kuhakikisha kinakamilika kwa wakati kutokana na kuchelewa kulikosababishwa na sababu mbalimbali.
Prof. Mbarawa ameyasema hayo jana alipotembelea kwa lengo la kukagua mradi huo wa upanuzi na ukarabati wa Kiwanja cha Ndege Kigoma ikiwa ni sehemu ya mradi wa viwanja vinne ambapo viwanja vingine ni Tabora,Shinyanga na Sumbawanga vyote vikigharimu kiasi cha Shilingi Bilioni 46.6.
" Wananchi wa Kigoma wamesubiri maboresho ya kiwanja hiki kwa muda mrefu hivyo tumsukume mkandarasi kufanya kazi usiku na mchana ili kazi imalizike haraka iwezekanavyo," Amesema Mbarawa.
Pamoja na hayo Prof. Mbarawa amemuagiza mtendaji mkuu wa Wakala wa Barabara (Tanroads) kusimamia ubora katika ujenzi wa kiwanja hicho pamoja na kuharakisha uagizaji wa vifaa vya kukamilisha ujenzi wa jengo la abiria ili kutokwamisha kasi ya ujenzi huo.
Kwa upande wake Mkuu wa Mkoa wa Kigoma Thobias Andengenye amesema wameupokea mradi huo kwa furaha na shauku kubwa na kuahidi kutoa ushirikiano kadri unatakavyohitajika kusaidia mradi kukamilika na kuanza kutumika.
Aidha Mhandisi wa Mradi kutoka Tanroads Donatus Binemungu amesema kwa siku za karibuni hali ya mvua imekuwa kikwazo cha kasi ya ujenzi huku akieleza kuwa ujenzi wa jengo la abiria umefikia asilimia 50 na ujenzi wa mnara wa kuongozea ndege ukiwa kwenye hatua nzuri zaidi.
Social Plugin