Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

SAMIA LEGAL AIDS CAMPAIGN KUENDELEA KUTOA MSAADA WA KISHERIA KWA WANANCHI

 

Na Dotto Kwilasa,Dodoma

Serikali imesema licha ya elimu inayotolewa kwa wananchi kuhusu masuala mbalimbali ya kisheria,bado kuna changamoto za uelewa wa kisheria katika jamii ikiwemo kwenye ukatili wa kijinsia,migogoro ya ardhi, ndoa na ardhi. 

Waziri wa Katiba na Sheria,Dk Damas Ndumbaro ameeleza hayo Jijini Dodoma leo January 20,2025 wakati akizungumza na waandishi wa habari na kueleza kuwa kupitia kampeni ya Mama Samia Legal Aids Compain (MSLAC) mikoa Sita itafikiwa kwa ajili ya uelimishaji.

Amesema kupitia MSLAC wamebaini kuwa kwenye sekta ya ardhi kuna ubabaishaji  mwingi jambo linalozua migogoro mingi na kumwomba Waziri wa Ardhi,Deogratius Ndejembi kumtumia orodha ya migogoro sugu ili baada ya kampeni hiyo waanze kuishughulikia.

"Kupitia kampeni hiyo tulifika katika mikoa 11 na changamoto zilizojitokeza kwa wingi ni  ukatili wa kijinsia,migogoro ya ardhi, ndoa na ardhi,katika sera yetu ya utoaji haki tutahakikisha  wananchi wanapata haki na wanapata elimu ya kisheria,"amesema.

Amesema watu wa pembezoni wana kiu ya haki ndio maana Rais aliunda Tume ya Haki jinai ambayo ilibainisha umuhimu wa haki kumfikia kila Mwananchi.

"Kupitia kampeni hiyo tuliweza kuwafikia watu  175,119 ambapo  asilimia 49 ni  wanawake na 51 ni wanaume ambapo tulitatua jumla ya migogoro  3162,takwimu hizi zinaonesha wanaume ni wengi kuliko wanawake ni takwimu nzuri tu,unaona Mpango huu unamsaidia Mwananchi kuzalisha zaidi, programu hii ni mkombozi kwa wanyonge hasa wale ambao hawana uwezo wa kupata mawakili,"amesema Waziri Ndumbaro

Waziri huyo pia amesema mpango huo utamsaidia mnyonge kupunguza malalamiko katika sekta ya sheria na kwamba  Januari 24 mwaka huu watazindua kampeni hiyo kwa mikoa 6 Mkoani Kigoma.

"Mikoa mingine itakayofikiwa ni,Kilimanjaro,Geita,Katavi,Tabora na Mtwara,katika mikoa hiyo tutakuwa Januari tu na  katika Kila Halmashauri wataenda Kata 10 katika Kila Kata watatumia siku 9 na huduma  zitatolewa bure kwa wananchi,"amesema 



Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com