CHINI ya uongozi wa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan, Tanzania imeendelea kuimarisha upatikanaji wa nishati kwa wananchi kupitia miradi mikubwa kama Bwawa la Nyerere (JNHPP), ambalo linalenga kuzalisha zaidi ya megawati 2,115, pamoja na uwekezaji katika nishati mbadala kama umeme wa jua na upepo.
Tanzania pia ni mwenyeji wa Mission 300 Africa Energy Summit, itakayofanyika Januari 27-28 , 2025 jijini Dar es Salaam.
Tukio hili linakusudia kuharakisha upatikanaji wa nishati kwa wote barani Afrika, huku likisisitiza ushirikiano wa kimataifa na suluhisho endelevu.
Kwa jitihada hizi, Tanzania inathibitisha nafasi yake kama kinara wa maendeleo ya nishati Afrika, ikizingatia maendeleo ya kiuchumi, kijamii, na uhifadhi wa mazingira.
Social Plugin