Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

VETA MKINGA YAPONGEZWA KUSHIRIKIANA NA WANANCHI KIMAENDELEO


Na Hamida Kamchalla, MKINGA.


WANANCHI wilayani Mkinga Mkoa wa Tanga wamesisitizwa kutumia fursa ya kuwapeleka vijana wao katika Chuo cha Utundi Stadi (VETA) ili kunufaika na mafunzo yanayotolewa.


Mbali na vijana kupatiwa mafunzo na kufanikiwa vizuri, pia wamekuwa msaada mkubwa katika kusaidia mambo mbalimbali jamii zinazowazunguka ikiwa ni pamoja na kushirikiana nao katika shughuli za kiuchumi.

Akiwakilishwa na Ofisa Tarafa ya Mkinga Heugen Mkinga ameyasema hayo kwenye maadhimisho ya miaka 50 ya Ufundi Stadi na miaka 30 ya VETA katika viwanja vya chuo hicho.

Aidha amesema chuo cha Ufundi Stadi (VETA) Wilaya ya Mkinga mbali na mafunzo mbalimbali yanayotolewa kimekuwa kikiimarisha shughuli zinazofanywa na wananchi wa Wilaya hiyo kwa kuongeza thamani madini ya mawe.

Mkuu wa Wilaya hiyo Gilbert Kalima amesema ipo haja ya kuupongeza uongozi wa Chuo hicho kwani kimekuwa kikiongeza kipato kwa wananchi kupitia madini hayo yanayojulikana kama, Tanga Stone.

"Nipende kuupongeza uongozi wa chuo hiki kwa kuboresha kazi ambazo zinafanywa na wananchi hasa katika kuongeza thamani madini ya mawe ya Tanga Stone ambayo yanapatikana wilayani hapa,

"Kwa kuongeza thamani, tunakwenda kuongeza kipato na kuwainua wananchi wa Mkinga ambao wanatapa tabu nyingi sana kuyatafuta mpaka kutapata hayo mawe" amesema Kalima.

Kalima amebainisha kwamba yapo mambo ya kujivunia ambayo yanaonekana kupitia Chuo hicho kwa kuzalisha vijana ambao tayari wameshakuwa msaada mkubwa kwa jamii zinazowazunguka.

Amesema wapi vijana wapatao 50 ambao wamekuwa wakisaidia shughuli mbalimbali ikiwemo ya kuwaunganishia wananchi umeme bila tozo ni kama kurudisha fadhila kwa wananchi hao.

"Ndugu zangu, kwa Mkinga vijiji 85 vimeshasambaziwa umeme bado vitongoji, ni imani yangu wale vijana 50 wanaosomeshwa hapa kuwasaidia wananchi na kutatua kero walizokuwa wanazipata,

"Awali kabla chuo hiki hakijajengwa hapa tulikuwa tunaeafuata mafunfi umeme kutoka Wilaya ya Tanga, lakini tuna imani wananchi watakwenda kuipata huduma ile kwa karibu na kwa wakati", amesema.

Naye Mkuu wa Chuo hicho Kalvin Haule amesema chuo kina uwezo wakudahili wanafunzi 240 wa mafunzo ya muda mrefu, ambapo 144 nlwanaishi katika mabweni ya chuo na 96 wa kuwa, kati yao 88 wa kiume na 64 wa kike.

"Lakini pia tunatoa mafunzo ya muda mfupi ambapo chuo kinadahili wanafunzi wapatao 100 kwa mwaka kwa kuzingatia mahitaji ya shuhuli za kiuchumi kwa Wilaya ya Mkinga" amesema Haule.

Haule amefafanua kwamba kwa sasa chuo kinatoa mafunzo ya muda mrefu ya aina tatu, ambayo ni umeme wa majumbani, uungaji na uchomeleaji vyuma pamoja na ushonaji na Teknolojia ya nguo.


Hata hivyo baadhi ya wanafunzi chuoni hapo wamesema yapo mengi ya kujifunza na kwamba hata kwa wanaoshindwa kuendeleza na masomo ya upili bado wana nafasi kubwa ya kupata ustadi na kuelekea kupata ajira.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com