Katika maandalizi ya Kongamano la Afya ya Akili Tanzania 2025 yanayoendelea, Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Women and Youth Development Solution (WAYDS), Bw. Charles Deogratius, na Meneja wa Programu, Bi. Thereza John, wamefanya kikao na Timu ya Usimamizi wa Afya ya Mkoa wa Shinyanga (RHMT) leo Jumatatu, Januari 20, 2025.
Mkutano huo umeongozwa na Mganga Mkuu wa Mkoa, Dr. Yudas Ndungile ukiwa na lengo la kufanikisha maandalizi ya Kongamano la Afya ya Akili la Tanzania, litakalofanyika Machi 2025 katika Manispaa ya Kahama, Mkoa wa Shinyanga
Kongamano hilo linatarajiwa kuwa jukwaa muhimu la kukutanisha wadau mbalimbali wakiwemo viongozi wa serikali, wataalamu wa afya na wadau mbalimbali wa afya ya akili kwa ajili ya kujadili na kupanga hatua za pamoja za kuboresha mifumo ya afya ya akili nchini Tanzania.
Kongamano hili litalenga hasa ushiriki wa vijana na umuhimu wa suluhisho za kijamii katika kutatua changamoto za afya ya akili, huku likijumuisha majadiliano, uwasilishaji, na warsha zitakazozungumzia matatizo ya afya ya akili yanayoikumba Tanzania.
Fursa za Kushiriki:
Usajili wa Vijana kama Wajumbe wa Kongamano
Vijana wa Tanzania wenye hamu ya kuwa mabalozi wa afya ya akili wanakaribishwa kujiandikisha kwa nafasi za wajumbe wa kongamano wenye udhamini. Hii ni fursa muhimu ya kushiriki katika majadiliano na kuwa sehemu ya suluhisho katika masuala ya afya ya akili nchini.
Jiandikishe Hapa kwa Nafasi za Wajumbe wa UdhaminiOnyesha Programu Bora za Kijamii
Taasisi na watu binafsi wanaoendesha programu bunifu za kijamii zinazolenga matatizo ya afya ya akili wanakaribishwa kuwasilisha juhudi zao katika kongamano hili. Hii ni nafasi nzuri ya kushiriki mafanikio yako na kuwahamasisha wengine kufanya kazi katika sekta hii.
Tuma Programu Yako HapaMaombi ya Kujitolea kwa Vya Habari
Ikiwa ungependa kusaidia katika utangazaji wa kongamano hili, unaweza kujiunga kama mjumbe wa kujitolea katika vyombo vya habari. Hii ni njia nzuri ya kusaidia kueneza ujumbe wa kongamano na kuwa sehemu ya kampeni ya kitaifa ya afya ya akili.
Jitolee Hapa
Ushirikiano wa Pamoja kwa Afya ya Akili
Mradi huu, unaoendeshwa na WAYDS na kufadhiliwa na Fondation Botnar, unaonesha dhamira ya kutatua changamoto za afya ya akili katika ngazi za mkoa na taifa. Kongamano hili linatarajiwa kuwa ni mkusanyiko wa wadau wa sekta ya afya ya akili, litakalosaidia kutengeneza suluhisho endelevu kwa matatizo ya afya ya akili nchini Tanzania.
Kwa taarifa zaidi na kwa jinsi ya kushiriki, tafadhali fuatana na WAYDS na mitandao rasmi ya kongamano hili.
Social Plugin