{ "@context": "https://schema.org", "@graph": [ { "@type": "Organization", "@id": "https://www.malunde.com/#organization", "name": "Malunde 1 Blog", "url": "https://www.malunde.com/", "logo": { "@type": "ImageObject", "url": "https://blogger.googleusercontent.com/img/a/AVvXsEgn0novZbFC67mK2Bal0GLeaysWSE_7JlLLeR7XBpCAh8u0Xyu4glbc96ptmIwK3Ttiz1w9ZSDe1WzDDJLEzxk0mAPPSAMbTFrJhhotrBSoLjJuIGyyO3ODi8k7mYTfPAl7uu9zxFF--xEJwZzlnsDBAF1oHiPC2C8DTHiSHFMBy_mWFIQK4c3ebTXhlg=s720" }, "sameAs": [ "https://www.facebook.com/malundekadama", "https://www.instagram.com/malundeblog", "https://x.com/malundekadama" ] }, { "@type": "WebSite", "@id": "https://www.malunde.com/#website", "url": "https://www.malunde.com/", "name": "Malunde 1 Blog", "description": "Habari, Matukio, Burudani, Nyimbo za asili, Siasa, Utamaduni, Mahusiano na Michezo kutoka Tanzania", "publisher": { "@id": "https://www.malunde.com/#organization" } }, { "@type": "BreadcrumbList", "@id": "https://www.malunde.com/#breadcrumb", "itemListElement": [ { "@type": "ListItem", "position": 1, "name": "Home", "item": "https://www.malunde.com/" } ] } ] } WAKAZI 6,000 NAMTUMBO KUNUFAIKA NA MRADI WA MAJI SAFI

Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

WAKAZI 6,000 NAMTUMBO KUNUFAIKA NA MRADI WA MAJI SAFI


Baadhi ya wakazi wa kitongoji cha Dodoma kata ya Ligera Wilayani Namtumbo wakiangalia Tenki la kuhifadhia maji ambalo litatumika kwa ajili ya kusambaza huduma ya maji wilayani humo
Tenki lenye uwezo wa kuhifadhi lita 10,000 za maji Wilayani Namtumbo
Mhandisi wa Maji kutoka Ofisi ya Meneja wa RUWASA Wilaya ya Namtumbo Mkoani Ruvuma Salome Method kushoto akiwaonyesha kisima cha maji baadhi ya wakazi wa kitongoji cha Dodoma Kata ya Ligera Wilayani Namtumbo.
Na Regina Ndumbaro-Namtumbo.

Zaidi ya wakazi 6,000 wa vijiji vya Kilimasera, Ukiwayuyu, Mtakanini, Mterawamwahi, na Matependwe katika Halmashauri ya Wilaya ya Namtumbo mkoani Ruvuma wanatarajia kuondokana na changamoto ya muda mrefu ya upatikanaji wa maji safi na salama. 

Serikali imeipatia Wakala wa Maji na Usafi wa Mazingira Vijijini (RUWASA) wilayani humo Shilingi milioni 300 kwa ajili ya kutekeleza uchimbaji wa visima virefu vitano kama sehemu ya mpango wa kuchimba visima 900 kwa kila jimbo.

Kaimu Meneja wa RUWASA Wilaya ya Namtumbo, Salome Method, amesema kuwa kazi ya uchimbaji wa visima hivyo ilianza Oktoba 2024 na inatarajiwa kukamilika mwishoni mwa Februari 2025. 

Kazi zilizopangwa ni pamoja na uchimbaji wa visima, ujenzi wa vioski vya kuchotea maji, ujenzi wa mfumo wa usambazaji maji, uwekaji wa matenki yenye uwezo wa kuhifadhi lita 10,000 kwa kila kijiji, ufungaji wa pampu za kusukuma maji, pamoja na mifumo ya umeme wa jua (solar power).

Kwa mujibu wa Method, hadi sasa uchimbaji wa visima na ununuzi wa vifaa muhimu umekamilika, huku ujenzi wa vioski vya kuchotea maji ukiwa umefikia zaidi ya asilimia 80. 

Pia amepongeza juhudi za Rais Samia Suluhu Hassan kwa kutoa fedha za utekelezaji wa miradi hii muhimu, ambayo itaongeza upatikanaji wa maji safi na salama wilayani Namtumbo kutoka asilimia 71 hadi 74.

Diwani wa Kata ya Ligera, Somebody Mhongo, ameishukuru serikali kwa kufanikisha mradi wa kisima cha maji katika Kitongoji cha Dodoma, Kijiji cha Mterawamwahi, ambacho kwa muda mrefu wakazi wake wamekuwa wakitegemea maji kutoka kwenye mabonde na mito ambayo siyo safi. 

Naye Mtendaji wa Kijiji cha Mterawamwahi, Joseph Haule, amesema kuwa kijiji hicho kimekuwa na changamoto kubwa ya maji, kwani kinategemea mabomba mawili ya kupampu kwa mkono ambayo hayakidhi mahitaji ya wakazi wake.

Baadhi ya wakazi wa kitongoji hicho wameeleza kuwa uhaba wa maji umesababisha changamoto mbalimbali, ikiwemo migogoro ya ndoa kutokana na wake zao kuchelewa kurudi nyumbani wakitafuta maji. 

Mkazi mmoja, Lucy Mgala, amesema kuwa wanawake hulazimika kwenda kuchota maji mtoni na mabondeni, hali inayowasababisha kupata madhara hasa wakati wa masika kutokana na utelezi wa barabara.

Kamenya Kawina, mkazi mwingine wa kitongoji cha Dodoma, amesema kuwa kwa sasa wanatembea kilomita moja kila siku kwenda kuchota maji, jambo ambalo linapoteza muda mwingi na kuathiri maendeleo yao kiuchumi. 

Amesema kuwa iwapo mradi huo utakamilika haraka, wananchi wataweza kupata muda wa kujikita katika shughuli za uzalishaji mali badala ya kutumia muda mwingi kutafuta maji.

Wananchi wa eneo hilo wameiomba serikali kupitia RUWASA kuhakikisha mradi huo unakamilika kwa wakati ili waweze kupata huduma ya maji safi karibu na makazi yao. 

Wamesisitiza kuwa upatikanaji wa maji safi utachangia kuboresha maisha yao kwa ujumla, afya zao, na kukuza maendeleo ya kijamii na kiuchumi katika vijiji vyao.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com