Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

DKT. DAMAS NDUMBARO AMFARIJI MAMA ALIYEONDOKEWA NA MWANAE


Na Regina Ndumbaro - Songea

Waziri wa Katiba na Sheria na Mbunge wa Jimbo la Songea Mjini, Mheshimiwa Dkt. Damas Ndumbaro, leo Februari 13, 2025, amemtembelea na kumfariji Bi. Zauna Haule, Mjumbe wa Kamati ya Siasa ya Kata ya Mjimwema, aliyefiwa na mtoto wake katika Manispaa ya Songea.

 Mheshimiwa Dkt. Ndumbaro ametoa pole kwa familia ya Bi. Haule na kuwasihi kuwa na subira katika kipindi hiki kigumu cha majonzi. 


Amesisitiza umuhimu wa jamii kushikamana na kuunga mkono familia zinazopitia changamoto kama hizi.


"Nimekuja kutoa pole kwa msiba huu mzito uliomkuta Bi. Zauna Haule na familia yake. Ni wajibu wetu kama viongozi na wanajamii kuwa karibu na wafiwa katika nyakati kama hizi," amesema Dkt. Ndumbaro.

Bi. Haule ametoa shukrani kwa Mheshimiwa Dkt. Ndumbaro kwa kujitokeza na kuwafariji katika kipindi hiki cha huzuni.

 Ameeleza kuwa uwepo wa viongozi na wanajamii umewapa faraja kubwa na kuwapa nguvu ya kuendelea mbele licha ya majonzi waliyonayo.

Viongozi wengine wa kisiasa na kijamii wa Manispaa ya Songea pia wamehudhuria kutoa pole kwa familia ya Bi. Haule. 
   

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com