
Haya yalitokea baada ya Onyancha kupokelewa kwa mangumi na mateke kutoka kwa mkuu wa shule kwa kuchelewa kuripoti shuleni.
Mwalimu huyo aliambia Citizen Digital kwamba bosi wake alimvamia mbele ya wanafunzi alipokuwa akifundisha darasani.
"Alinipiga teke na kofi. Kisha akanibburuta hadi ofisini kwake ambako aliendelea kunishambulia," mwalimu huyo alisema.
Baadaye mwalimu huyo alipelekwa katika hospitali ya mtaa wa Ikonge, ambako anaendelea na matibabu ya majeraha aliyoyapata kutokana na kushambuliwa.
Akisimulia kisa hicho, maafisa wa Muungano wa Walimu wa Elimu ya baada ya Shule ya Msingi (KUPPET) wamelaani shambulio la mkuu wa shule dhidi ya mwalimu huyo na kutaka hatua za kisheria zichukuliwe dhidi yake.
Viongozi hao walionya kuwa walimu watagoma iwapo hakuna hatua zitakazochukuliwa dhidi ya mkuu wa shule hiyo.
Social Plugin