Akizungumza baada ya kuchaguliwa amesema anahitaji kwenda kubadilisha klabu hiyo ikiwemo masuala ya nidhamu kwani ndiyo Msingi wa Maendeleo
Matokeo hayo, yametangazwa na Mwenyekiti wa Kamati huru ya uchaguzi Wakili wa Kujitegemea, Raphael Awino katika uchaguzi uliofanyika mapema leo Februari 28, 2025, kwenye ukumbi wa mikutano wa Anatouglo, Ilala mjini Dar e salaam.
Kwa upande wa Makamu Mwenyekiti, Mary Geoffrey, ameibuka na kura 70 za ndiyo na saba za hapana na nne zimeharibika.
Kwa upande wa Wajumbe watano, waliochaguliwa ni Selemani Jongo (69), Penina Malundo (62), Andrew Msechu (67) na Khamis Miraji (59) na Veronika Mrema (69).
Uchaguzi umefanyika kwa Amani na utulivu, jambo ambalo Mwenyekiti wa Tume ya uchaguzi Raphael Awino amelisifu kuwa la mfano.
Naye Katibu wa Tume Huru ya uchaguzi, Janet Jovin amepongeza pia kwa uchaguzi uliofanyika kwa Amani.
Social Plugin