Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

MKUU WA WILAYA YA MASASI ASISITIZA MAZOEZI KWA WATUMISHI WA UMMA


Mkuu wa Wilaya ya Masasi Lauter J Kanoni akifanya mazoezi na watumishi wa umma wilayani Masasi

Baadhi ya watumishi wakifanya mazoezi hayo
Katibu Tarafa wilaya ya Masasi bi Irene Mbwana akizungumza namna mazoezi hayo ni muhimu kwa afya ya mwanadamu
Picha ya pamoja ya Mkuu wa Wilaya ya Masasi Lauter J Kanoni na watumishi wa wilaya hiyo

Na Regina Ndumbaro-Masasi. 

Mkuu wa Wilaya ya Masasi, Mheshimiwa Lauter John Kanoni, amesisitiza umuhimu wa mazoezi kwa watumishi wa umma ili kuboresha afya na kuongeza ufanisi katika kazi. 

Ameyasema hayo aliposhiriki katika jogging maalum iliyoandaliwa kwa watumishi wa wilaya hiyo, akisisitiza kuwa mazoezi ni nyenzo muhimu kwa maendeleo ya mtumishi na taasisi kwa ujumla.

Katika hotuba yake, Kanoni amewataka watumishi wa umma kutenga muda wa kufanya mazoezi mara kwa mara ili kuboresha afya zao na kujikinga na magonjwa yasiyoambukiza. 

Amesema kuwa mazoezi husaidia kuongeza morali kazini, kuimarisha mahusiano baina ya watumishi, na kujenga mshikamano katika taasisi mbalimbali.

Mkuu huyo wa wilaya ameeleza kuwa kupitia jogging kama hii, watumishi wa umma wanapata nafasi ya kufahamiana zaidi na kuimarisha ushirikiano kazini. 

Aidha, amesisitiza kuwa watumishi wenye afya njema huweza kutoa huduma bora kwa wananchi, hivyo ni muhimu kufanya mazoezi kama sehemu ya maisha ya kila siku.

Katika tukio hilo, Kanoni amezindua kauli mbiu ya jogging hiyo kuwa "Michezo ni Afya Bora kwa Watumishi", amewahimiza wote kuichukua kwa uzito na kuendelea kushiriki katika mazoezi mara kwa mara. 

Amesema kuwa kauli mbiu hiyo inapaswa kuwa mwongozo wa kila mtumishi katika kuhakikisha wanadumisha afya njema kwa ajili ya ufanisi wa kazi zao.

Kwa upande wake, Katibu Tarafa wa Masasi, Bi. Irene Mbwana, amewashukuru watumishi wa umma na washiriki wa jogging kwa kujitokeza kwa wingi kumuunga mkono Mkuu wa Wilaya katika tukio hilo. 

Amesema kuwa kitendo cha kushiriki mazoezi kwa pamoja ni ishara ya mshikamano na utayari wa kujenga afya bora kwa manufaa ya wote.

Bi. Irene amewahimiza watumishi wa umma kuendelea kujenga utamaduni wa kufanya mazoezi mara kwa mara ili kuepuka magonjwa yanayotokana na mtindo wa maisha usiofaa. 

Amesisitiza kuwa mazoezi siyo tu yanaboresha afya, bali pia yanasaidia kupunguza msongo wa mawazo na kuimarisha ufanisi kazini.

Washiriki wa jogging hiyo walionekana kuwa na shauku kubwa ya kushiriki mazoezi hayo na walitoa pongezi kwa Mkuu wa Wilaya kwa kuwahamasisha. 

Wameeleza kuwa tukio hilo limewasaidia kuona umuhimu wa mazoezi na wako tayari kuendeleza utamaduni huo.

Jogging hiyo imehitimishwa kwa mazungumzo ya pamoja ambapo watumishi wameeleza kuwa wataendelea kushiriki katika mazoezi kama sehemu ya maisha yao ya kila siku. 

Mkuu wa Wilaya ameahidi kuwa jogging kama hiyo itakuwa endelevu ili kuhakikisha afya za watumishi wa umma zinaimarika na wanakuwa na utendaji kazi mzuri.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com