
Na Hamida Kamchalla, TANGA.
RAIS Dkt. Samia Suluhu Hassan ili kukabiliana na tatizo la ukosefu wa ajira kwa vijana mkoani Tanga, serikali ina mpango wa baadae kufanya bandari ya Tanga kuwa maalumu ili kazi ziwe nyingi na kuongeza ajira.
Rais aliyasema hayo leo akiongea na wananchi wa Mkoa wa Tanga kwenye mkutano wa hadhara, katika uwanja wa Ccm Mkwakwani jijini Tanga.
Amebainisha kwamba boreshwaji wa bandari ya Tanga umeanza kupunguza tatizo la ajira kwa vijana, lakini jitihada zaidi zinafanyika kumaliza tatizo hilo.
"Serikali ina mpango wa baadae kufanya bandari ya Tanga kuwa ni maalumu kwa ajili ya kilimo, kazi zitakuwa nyingi na ajira zitaongezeka kwa vijana, wasiwe wanakaa bila kazi na kuishia kwenye vijiwe vya kahawa kupiga majungu" amesema.
Hata hivyo alieleza changazoto alizozikuta kwenye baadhi ya maeneo wakati wa ziara yake kwamba ni miundombinu ya barabara na maji ambavyo tayari serikali inashuhulika navyo.
Lakini pia alisema wakati wa ziara hiyo alikuta miradi ambayo haijakwisha hivyo aliagiza Maofisa masurufu kusimamia miradi ambayo haijamalizika.
Mbunge wa Jimbo la Tanga Ummy Mwalimu kwa niaba ya wananchi aliiomba serikali kufufua viwanda ambayo miaka ya nyuma vilikua ndiyo tegemeo la vipato vya wananchi walio wengi.
"Tanga ya miaka ya 80 ilikuwa ya viwanda na ilikuwa inashika nafasi ya pili ikiongozwa na Dar es salaam, Mh. Rais, tunaomba utufufulie viwanda kwa manufaa ya wananchi wetu, vijana wapate ajira ili waendeshe maisha yao" alisema.
Lakini pia mbunge huyo alibainisha kwamba kutokana na jiografia ya jiji la Tanga zipo baadhi ya kata ambazo zipo nje ya mji, hivyo nao wanastahili kupelekewa umeme wa REA kama ilivyo kwa vijiji vingine vya wilayani.

Social Plugin