Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

SERIKALI NA WADAU KUSHIRIKI MKUTANO WA KITAIFA WA AFYA YA AKILI KITAIFA MKOANI SHINYANGA



Kikao cha maandalizi ya mkutano wa Kitaifa wa Afya ya Akili unaotarajiwa kufanyika katika wilaya ya Kahama, mkoani Shinyanga,Mwezi Mei 30 hadi 31, 2025 kikiendelea .

Na Mwandishi wetu - Malunde 1 Blog.

Mkutano wa Kitaifa wa Afya ya Akili unatarajiwa kufanyika katika wilaya ya Kahama, mkoani Shinyanga, kuanzia Mei 30 hadi 31, 2025 ukihusisha wadau mbalimbali kutoka ndani na nje ya nchi, wakiwemo wataalamu wa afya ya akili, ili kujadili kwa pamoja changamoto na ufumbuzi kuhusu tatizo la afya ya akili, ambalo limekuwa ni changamoto kubwa katika Taitaifa.

Akizungumzia maandalizi ya mkutano huo Mwenyekiti wa Kamati ya Maandalizi, Faustine Mlyutu,leo, Februari 21, 2025, amesema kuwa mkutano huo unalenga kukutanisha zaidi ya watu 500, kwa lengo la kujadili madhara yatokanayo na changamoto ya afya ya akili na jinsi ya kupunguza changamoto hiyo.

Aidha Mlyutu amebainisha kuwa mkutano huo ni hatua muhimu katika kuimarisha elimu na ufahamu kuhusu afya ya akili na kuleta mabadiliko chanya kwa jamii juu ya changamoto hiyo.

Awali Mkurugenzi wa Shirika la WAYDS, Charles Deogratius, linaloshiriki katika maandalizi ya mkutano huo, amesema tatizo la afya ya akili ni ugonjwa kama magonjwa mengine huku akiwaomba wadau wengine kushirikiana kuondoa unyanyapaa dhidi ya watu wenye matatizo ya afya ya akili.

Kwa upande wake Kaimu Meneja Mpango wa Magonjwa yasiyoambukiza kutoka Wizara ya Afya, Edith Bakari, ameeleza kuwa faida ya mkutano huo ni kujenga mashirikiano baina ya serikali na wadau ili kuanzisha mpango wa pamoja wa kupambana na tatizo la afya ya akili nchini huku Christiani Alais kutoka Hospitali ya Taifa ya Afya ya Akili ya Milembe mkoani Dodoma, akieleza kuwa kila mwaka hospitali hiyo hupokea wagonjwa 50,000 wa afya ya akili.Mwenyekiti wa Kamati ya Maandalizi, Faustine Mlyutu,akiongoza kikao cha maandalizi ya mkutano wa Kitaifa wa Afya ya Akili unaotarajiwa kufanyika katika wilaya ya Kahama, mkoani Shinyanga, kuanzia mwezi Mei 30 hadi 31, 2025Wadau wa mkutano wa Kitaifa wa Afya ya Akili wakiendelea na kikao.Mkurugenzi wa Shirika la WAYDS, Charles Deogratius,akielezea maandalizi kuelekea mkutano huo.Wadau wa mkutano wa Kitaifa wa Afya ya Akili unaotarajiwa kufanyika katika wilaya ya Kahama, mkoani Shinyanga, wakiendelea na kikao.Wadau wa mkutano wa Kitaifa wa Afya ya Akili unaotarajiwa kufanyika katika wilaya ya Kahama, mkoani Shinyanga, wakiendelea na kikao.
Wadau wa mkutano wa Kitaifa wa Afya ya Akili unaotarajiwa kufanyika katika wilaya ya Kahama, mkoani Shinyanga, wakiendelea na kikao.
Wadau wa mkutano wa Kitaifa wa Afya ya Akili unaotarajiwa kufanyika katika wilaya ya Kahama, mkoani Shinyanga,
Wadau wa mkutano wa Kitaifa wa Afya ya Akili unaotarajiwa kufanyika katika wilaya ya Kahama, mkoani Shinyanga, wakiendelea na kikao.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com