Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

MAAFISA WA CCM WILAYA YA MASASI WAPEWA SEMINA YA UONGOZI

Makatibu na Kata wakiendelea kusikiliza maelekezo ya elimu kutoka kwa katibu wa Chama Cha Mapinduzi CCM Mkoa Comrade Abuu Athuman Yusuf
Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana  Chama cha Mapinduzi (UVCCM) Mkoa wa Mtwara Comrade Abuu Athuman Yusuf akiongoza semina hiyo ya kutoa elimu kwa makatibu CCM

Na Regina Ndumbaro-Masasi. 

Chama cha Mapinduzi (CCM) Wilaya ya Masasi kimeandaa semina maalum kwa makatibu wa kata, matawi, na jumuiya zote za chama wilayani humo. 

Semina hiyo imelenga kuwajengea uwezo wa uongozi ili kuhakikisha utekelezaji wa majukumu ya chama unafanyika kwa ufanisi na nidhamu ya hali ya juu.

Semina hiyo imeendeshwa na Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana wa CCM (UVCCM) Mkoa wa Mtwara, Comrade Abuu Athuman Yusuf ambae aliteuliwa na CCM makao makuu kuongoza mafunzo hayo. 

Katika hotuba yake ya ufunguzi, Comrade Abuu amesisitiza umuhimu wa makatibu wa kata na matawi kuwa mstari wa mbele katika kuhamasisha wanachama na wananchi kushiriki katika shughuli za maendeleo.

Washiriki wa semina wamepata fursa ya kujifunza masuala muhimu yanayohusu uongozi, usimamizi wa shughuli za chama, na mbinu bora za kuimarisha mshikamano ndani ya CCM. 

Pia, wameelekezwa jinsi ya kusimamia shughuli za chama kwa kuzingatia katiba, kanuni, na maadili ya CCM.

Aidha, Comrade Abuu  amewahimiza makatibu hao kuhakikisha wanatekeleza majukumu yao kwa bidii na kuwa mfano bora kwa wanachama. 

Amesisitiza kuwa viongozi wa CCM wanapaswa kuwa na maadili mema, kuwa karibu na wananchi, na kuhakikisha wanashiriki kikamilifu katika kuimarisha chama kuanzia ngazi za chini.

Katika mjadala wa wazi uliofanyika baada ya mafunzo, washiriki wamepata nafasi ya kuuliza maswali na kutoa maoni yao kuhusu changamoto wanazokutana nazo katika utekelezaji wa majukumu yao. 

Baadhi ya changamoto zilizoibuliwa ni pamoja na upungufu wa rasilimali, ushirikiano mdogo kutoka kwa baadhi ya wanachama, na uhitaji wa mafunzo zaidi ya uongozi.

Viongozi wa CCM Wilaya ya Masasi wametoa shukrani kwa Comrade Abuu kwa uongozi wake mzuri katika semina hiyo na kuahidi kutekeleza mafunzo waliyopata kwa vitendo. 

Pia, wamesisitiza kuwa mafunzo kama haya yana mchango mkubwa katika kuhakikisha chama kinaendelea kuwa imara na kushinda chaguzi zijazo.

Semina hiyo imehitimishwa kwa mafanikio makubwa, huku washiriki wakiahidi kuwa mabalozi wa mabadiliko katika maeneo yao. 

Chama cha Mapinduzi kinaendelea kuwekeza katika mafunzo ya viongozi wake ili kuhakikisha kinaendelea kuwa chama imara chenye uwezo wa kusimamia maendeleo ya nchi kwa ufanisi.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com