Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

MFANYABIASHARA MAARUFU ,KADA WA CCM 'CHONCHORIO' APOTEA, ANATAFUTWA


Daniel Chonchorio Nyamhanga
Daniel Chonchorio Nyamhanga

Na Mwandishi Wetu, Mwanza

Mfanyabiashara wa jijini Mwanza, Daniel Chonchorio Nyamhanga, 46, ameripotiwa kutoweka katika mazingira ya kutatanisha baada ya kuaga familia yake asubuhi ya Jumapili Machi 23, 2025, kwamba anakwenda kufanya mazoezi ya viungo.
Chonchorio pia ni Mjumbe wa Mkutano Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Taifa mwenye makazi mengine katika mji wa Tarime mkoani Mara na jijini Dar es Salaam.

Taarifa iliyotolewa na Jeshi la Polisi Mkoa wa Mwanza jana Jumatatu inaeleza kuwa mfanyabiashara huyo, ambaye ni mkazi wa Mtaa wa Temeke katika kata ya Nyakato, wilayani Nyamagana aliondoka nyumbani kwake saa mbili asubuhi akiwa amevaa nguo za mazoezi na simu ya mkononi.

Wanafamilia wa Chonchorio walioripoti polisi tukio la kutoweka kwake walisema hadi kufikia muda wa saa tano asubuhi siku hiyo, ndugu yao hakurudi nyumbani hali iliyowafanya kuiingiwa wasiwasi na kulazimika kutoa taarifa kwa chombo hicho cha usalama wa raia na mali zao.

Taarifa inaeleza kuwa Jeshi la Polisi mara moja lilianza uchunguzi wa tukio hilo kwa kuwahusisha wanafamilia, ndugu, marafiki na majirani wa Chonchorio.

Hata hivyo, taarifa hiyo inaeleza kuwa hadi jana mfanyabiashara huyo alikuwa hajapatikana.

Chanzo - Mara Online News



Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com