
Akizungumza na Malunde 1 blog, saa chache baada ya kuchapisha taarifa ya uhitaji wa matibabu kwa mtoto huyo, Katambi amesema, "Nimeshashughulikia hili na mtoto atafanyiwa tiba muda wowote, punde nilipopata taarifa hizi. Nitamlipia gharama za upasuaji na nimeshaongea na uongozi wa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Shinyanga. Mtoto atapatiwa matibabu kuanzia sasa."
Mbunge Katambi amethibitisha kuwa hatua zote zimechukuliwa ili kuhakikisha mtoto huyo anapata matibabu bila kuchelewa, na kwamba gharama za upasuaji zitafidiwa na yeye binafsi.
Amesema atahakikisha mtoto huyo anapata huduma muhimu kwa haraka ili kuepusha madhara yoyote zaidi.
Mama wa mtoto, Naomi John, ameonesha furaha na shukrani kwa mbunge kwa msaada wa haraka aliotoa, na sasa mtoto wake atapata huduma ya matibabu ya haraka.
Soma habari ya Mwanzo
Social Plugin